“Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”
Bwana Yesu asifiwe. Karibuni tutafakari somo hili tulilopewa kuhusu utunzaji wa uumbaji wa Mungu.
“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi na nyimbo,tenzi za rohoni ,huku mkimwimbia Mungu kwa neema miongoni mwenu.”
Naomba tukumbushe kuwa Mungu ametuahidi mbingu mpya na nchi mpya baada ya kuiangamiza dunia iliyopo sasa yenye maovu na machukizo mengi kwa BWANA. Isaya 65:17 ‘’Maana tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya na mambo ya kwanza hayatakumbukwa,wala hayataingia moyoni. Lakini furahini mshangilie daima kwa ajili ya hivi niviumbavyo, maana tazama ,naumba Yesusalemu uwe shangwe na watu wake wawe furaha
Mungu ametuahidi ulinzi wa miili yetu na roho zetu.
Wakolosai 3:16. “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi na nyimbo,tenzi za rohoni ,huku mkimwimbia Mungu kwa neema miongoni mwenu.”
Katika maisha ya kawaida mkulima akishindwa kutambua majira ya mvua atachelewa kuandaa shamba, kupanda na kupalilia. Madhara ya jambo hilo ni kukosa mavuno na kama ni shamba la miti ya matunda atakosa matunda, kipato na chakula na hivyo kuingia katika shida ya njaa yeye na watoto wake au familia yake. Jambo hili litamnyima furaha na amani kwa kuwa atakuwa katika mahangaiko makubwa. Vivyo hivyo katika ulimwengu wa roho, kosa la kutotambua majira ya kujiliwa kwako yana madhara kwako na kwa watu wako.
“Ndipo akahuzunika na kusononeka.Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa, kaeni hapa mkeshe pamoja nami. Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, walakini sikama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe. Akawajia wale wanafunzi akawakuta wamelala, akawaambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja name hata saa moja? Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.
Mungu huinua vitu vinyonge au dhaifu au vilivyodharauliwa ili kuviaibisha vyenye nguvu vya dunia. Mungu anataka mwanadamu yoyote asije akajisifu mbele yake na ikiwa anaona fahari na aone fahari juu ya Bwana. Mungu anajitukuza kwa njia hii kwa kuwa yeye ndiye peke yake anayestahili kutukuzwa.
Katika somo hili tutaangalia mambo muhimu tunayopaswa kuzingatia tunapoamua kumfuata Bwana wetu Yesu Kristo na hatimaye kuwa wanafunzi wake. Mambo ya muhimu ya kuzingatia ni mengi lakini katika somo hili tutaangalia mambo muhimu matatu.
Tumeelezea kuwa katika tamaduni za Kipare kijana “anakuloka” pale anapofikia umri wa kuoa. Anatoka katika hatua ya ujana na kuingia katika hatua ya kuwa mtu mzima anayeweza kuruhusiwa na wazazi wake kuoa. Katika sehemu hii tutaangalia Neno la Mungu linasema nini kuhusu suala hili la “kukoloka”.