• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
  • 24 Nov, 2023
  • Admin


Naomba tukumbushe kuwa Mungu ametuahidi mbingu mpya na nchi mpya baada ya kuiangamiza dunia iliyopo sasa yenye maovu na machukizo mengi kwa BWANA.  Isaya 65:17 ‘’Maana tazama, mimi naumba mbingu mpya   na nchi mpya na mambo ya kwanza hayatakumbukwa,wala hayataingia moyoni. Lakini furahini mshangilie daima kwa ajili ya hivi niviumbavyo, maana tazama ,naumba  Yesusalemu uwe shangwe na watu wake  wawe furaha .Katika mstari ule wa  22 anasema BWANA, Kama vile mbingu mpya na nchi mpya nitakazofanya zitakavyokaa mbele zangu asema BWANA ,ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.Waraka wa pili wa Petro 3:7, 11-14  Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto kwa neno, lilohilo, zikilindwa hata siku ya hukumu na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu. Basi kwa kuwa vitu  hivi vyote vitafumuliwa hivyo imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu na kuihimiza ambayo  katika hiyo mbingu zitafunuliwa zikiungua na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka.Lakini kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya ,ambavyo  haki   yakaa ndani yake,kwa hiyo  wapenzi, kwa kuwa mnatazamia  mambo hayo, fanyeni bidii  ili mwonekane katika  amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.Ndipo mtakapofurahi sana katika BWANA nafsi zenu zitashangilia katika BWANA wenu,maana amewavika mavazi ya wokovu amewafunika mavazi ya haki kama bwana  harusi  ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi harusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu (Isaya 61:10). Roho wa Mungu  anayaambia makanisa kuwa kama umelishika neno lake atakulinda utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.Ufunuo 3:12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena  kabisa, nami  nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu,na jina langu mwenyewe lile jipya .Nao watamwona uso  wake na jina lake  litakuwa katika  vipaji vya nyuso zao.Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kitu change cha enzi,kama mimi  nilivyoshinda  nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha  enzi (Ufunuo 3:21) .Mungu wa amani mwenyewe awatakasa kabisa,nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe   kamili,bila lawama ,wakati wa kuja kwake Bwana wetu  Yesu Kristo (1 Wathesalonike 5:23).Mungu alibariki neno lake.Amina

Share This