Yohana Mtakatifu 17:3 “Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”
Maneno haya ni ya Bwana wetu Yesu Kristo akifundisha kuhusu uzima wa wa miliele unaopatikana katika kumjua Mungu wa pekee na wa kweli. Mungu wa pekee wa kweli ni Mungu aliyeziumba mbingu nan chi ma na vitu vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekan. Mungu pekee maana yake ni Mungu mmoja tu na hakuna mwingine wa kufanani9shwa naye huyu ndiye Mungu aliyeongea na Musa. Kutoka 6:2-3 “Kisha Mungu akasema na Musa akamwambia, Mimi ni YEHOVA, nami nilimtokea Ibrahimu na Isaka na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina la YEHOVA sikujulikana kwao.” Kutoka 3:14 “Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO, NDIVYO UTAKAVYOWAAMBIA WANA WA Israeli; MIMI NIKO amenitumia kwenu.” Huyu ndiye Mungu pekee wa kweli na baba wa vyote, badala yake hakuna kumbukumbu la Torati 6:4-5 “Sikiza, Ee Israeli, BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja. Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote,” watu wote wa ulimwengu wajue ya kuwa BWANA ndiye Mungu hakuna mwingine ila yeye. Waefeso 4:5 “Mungu mmoja; naye ni baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.” Huyu ndiye Mungu wa kweli ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu mwenye kuhimidiwa milele matendo ya mikono yake ni kweli vituongoze katika maisha yetu. Huyu ndiye Mungu tunayetakiwa tumjue ili tupate uzima wa milele. Mungu anataka tumfahamu na kumjua. Yeremia 9:24 “bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi na kunijua ya kuwa mimi ni BWANA, nitendaye wema, na hukumu na haki katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema BWANA.” Ukimjua Mungu utayajua mapenzi yake, yanayopatikana katika neno lake takatifu. Mungu wa kweli, Neno lake ni la kweli. Neno la Mungu ndio la kweli na kwelindio neno la Mungu linalotuweka huru kutoka dhambini. Uhuru wetu unategemea sana kukua kwetu katika kumjua Mungu, neno lake na njia zake. Yohana 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndiyo kweli.” Yesu Kristo Bwana wetu alipokuwa hapa duniani alifundisha iyo kweli ili watu wamjue Mungu wa kweli. Yohana 17:6-7 “Jina lako limewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako ukanipa mimi, na neno lako wamelishika sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa toka kwako. Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao nao wakayapokea.” Katika mstari huu wa Yohana 17:3 tunafunishwa kuwa uzima wa milele ni kumjua Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo aliyemtuma ulimwenguni. Kwa maneno mengine uzimz wa milele unapatikana kwa kumjua Mungu na mwanae pekee Yesu Kristo. 1 Yohana 5:11-13 “Na huu ndio ushuhuda ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele, na uzima huu umo katika mwanawe. Yeye aliyenae Mwana anao huo uzima, asiye naye mwna wa Mungu hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mamb hayo, ilimjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnao liamini jina la mwana wa Mungu.” Amwaminiye mwana yuna uzima wa milele, asiyemwamini mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia. Mungu alimtoa mwanae pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. Yohana 14:6-7 “Yesu akawaambia, mimi ndimi njia, na kweli, na uzima, mtu haji kwa baba, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua na Bsaba.” Kwa hiyo tunatakiwa kumjua Mungu na Mwanae Yesu Kristo, kupitia neno lake. Mtu akimpenda Bwana wetu Yesu Kristo, atalishika neno lake. Na Mungu baba atampenda nao watakuja kwake na kufanya makao kwake (Yohana 14:24-25). “Mtu asiyenipenda, yeye hasikii maneno yangu, nalo neno mlilolisikia sio langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.” Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishikati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu , ambaye alijitoa mwenyewe kwa ukombozi kwa ajili wote. Yohana 6:47 “Amin, amin nawaambia, yeye aaminie yuna uzima wa milele” mimi ndimi chakula cha uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki ataishi milele. Na chakula alichotoa ni mwili wake kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. Ndani yake ndimo kuna uzima, nao huo uzima ni nuru ya Ulimwengu. Neno lake ndiyo nuru ya ulimwengu inayotuweka huru. Yohana 8:31-32 “Basi Yesu akawaambia wale wayahudi waliomwamini, ninyi mkikaa katika neno langu, mmekiuwa wanafunzi wangu kwelikweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.” Basi mwana akituweka huru tutakua huru kutoka utumwa wa dhambi kwani kila atendaye dhambi nimtumwa wa dhambi. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. Tunatakiwa kumjua na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo kwa sababu anayo maneno ya uzima wa milele. Yohana 6:40 “£ kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye awe na uzima wa milele, name nitamfufua siku ya mwisho.” Mungu aliupenda ulimwengu ata akamtuma mwanaepekee Yesu Kristo ili tupate uzima wa milele kwa yeye 1 Yohana 4:10 “Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma mwanae kuwa kuipatanisho kwa dhambi zetu.” Kwa kuwa wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu tunatakiwa kutubu dhambi zetu na kuziacha na kuzaliwa kuwa viumbe wapya. 2 Wakorintho 5:17 “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kupya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya.” Ili tuweze kumjua Mungu wa kweli na mwanae aliyemtuma ni lazima tupate neema ya ufunuo kutoka kwaker. Waefeso 1:17-18 “Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima nay a ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru. Mjue tumaini la Kristo wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa uruthi wake katika watukufu jinsi ulivyo.” Hii inamaanisha kwamba hatuwezi kumjua Mungu ikiwa hatukuwa na mafunuo ya Roho Mtakatifu ndani yetu. Unahitaji Roho ya ufunuo ili kujua kilichofunuliwa kwanjia ya Neno la Mungu na kuliishi Neno hilo au kurithi. Watu wamjuao Mungu watakuwa hodari na kutenda mambo makuu kwa maana Roho Mtakatifu atawafunulia siri za Mungu. Maana Roho Mtakatifu huchunguza yote, hata mafunzo ya Mungu mambo ambayo jicho halikuona wa sikio halikusikia. Neno la Mungu linasema (1 Wakorontho 12:7) “Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.” Tumwombe Mungu atupe Roho mtakatifu wake ili atufunulie tumjue Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo aliyemtuma kwa ajili ya wokovu wetu na uzima wa milele.