KONDOO WASHIBE
Tuhakikishe kuwa tumewalisha kondoo hadi washibe kwa kuwafundisha kwa wingi neno la Mungu.Wakolosai 3:16. “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi na nyimbo,tenzi za rohoni ,huku mkimwimbia Mungu kwa neema miongoni mwenu.” Ujumbe wa Kristo ukikaa ndani yako Pamoja na utajiri wake wote unapata nguvu ya kumshinda shetani na hila zake zote .Mungu analiangalia neno lake ili alitimize.Amosi 8:11-12 “Angalia siku zinakuja asema Bwana Mungu ambazo nitaleta njaa katika nchi si njaa ya kukosa chakula ,wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana Nao watatangatanga toka bahari hata bahari na toka upande wa kaskazini hata upande wa mashariki,watapiga mbio,wakienda huko na huko kulitafuta neno la BWANA ,wasilione.” Tutumie vizuri wakati huu wa neema kufundishana neno la Mungu kwa wingi maadamu linapatikana kabla ya siku hizo mbaya hazijafika.
KONDOO WASITANGETANGE WALA KUTAWANYIKA
Tuhakikisha kuwa tuinawachunga kondoo wakae Pamoja zizini mwa BWANA wasitawanyike wala kutangatanga kulan a huku kwa kuwa huko nje kuna mbwa-mwitu wakali 1 Petro 5:8-9 “Mwe na kiasi na kukesha,kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye,huzunguka-zunguka,akitafuta mtu ammeza,Nanyi mpingeni huyo,mkiwa thabiti katika Imani,mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.” Basi tusilale usingizi kama wengine ,bali tukeshe na kuwa na kiasi, hali tukijivika kifuani Imani na upendo na chepeo yetu iwe tumaini la wokovu ,kwa Bwana wetu Yesu Kristo.Yakobo 4:7-8 “Basi mtiini Mungu .Mpingeni shetani,naye atawakaribia ninyi .Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yenu,enye wenye nia mbili.” Tuwaonye kwa upole na saburi wale wanaotanga-tanga huku na huko kwa maana wanahatari ya kukutana na mitume na manabii wa uongo na wadanganyifu .Mathayo 7:15-16 “Jihadhamini namanabii wa uongo watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa -mwitu wakali .Mtawatambua kwa matunda yao,Je watu huchuma zabibu katika miiba au tini katika mibaruti?” Mathayo Mtakatifu 24:4-5,24-26. “Yesu akajibu ,akawaambia,Angalieni,mtu asiwadanyanye.Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu,wakisema,Mimi ni Kristo nao watawadanganya wengi.Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo,ndo watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza, kama yamkini,hata walio wateule.Tazama nimekwisha kuwaonya mbele,Basi wakiwaambea,yuko jangwani, msitoke, yumo nyumbani, msisadiki.” Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na Imani wakisikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani (I Timotheo 4:1).Nneno la Mungu linatuonya kuwa tusiwe tena Watoto wachanga, tukitupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu kwa hila ya watu, kwa ujanja tukizifuata njia za udanganyifu maana watu kama hao ni mitume wa uongo watendao kazi kwa hila wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo .Wala si ajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano, wa watumishi wa haki ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao (2 Wakorintho 11:13-15) Nneno la Mungu linatufundisha kuwa tuishike kweli katika upendona kuku ahata tumfikie yeye katika yote yeye aliye kichwa Kristo.Tuyachunguze maandiko kama walivyofanya watu wa Benoya.Matendo ya Mitume 17:10-11 “Mara hao ndugu wakawapelelka Paulo na sila usiku hata Beroya.Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la wayahudi.Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike,kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo ,wakayachunguza maandiko kila siku ,waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.” Katika Waraka wa Kwanza wa Yohana 4:1-3 neno la Mungu linasema, “Wapenzi, msiiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani katika hili mwamjua Roho wa Mungu, kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mung una hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja na sasa imekwisha kuwako duniani.” Katika hili twamjua Roho wa kweli na roho ya upotevu.Roho mtakatifu ndiye Roho wa kweli, anayetongoza na kututia kwenye kweli yote kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe,lakini yote atakayoyasikia atayanena na mambo yajayo atutupasha Habari yake.
VIKUNDI VIDOGO VIDOGO
Bwana wetu Yesu Kristo aliagiza wanafunzi wake wawaketisha makutano vikao vikao kwa safu za watu mie na pengine watu hamsini ili kurahisisha uratibu na usimamizi wa makutano ilikila mmoja wao apate chakula cha kumtosha.Wakristo tunapokuwa kwenye vikundi vya jumuiya au “fellowship” tunapata wepesi wa kufundishana na neno la Mung una kujengana katika Imani.Tutatambua mafundisho yanayafaa kufundishwa katika kila kundi ili kuliimarisha.Waebrania 5:12-14”. Kwa maana,iwapopasapo kuwa walimu (maana wakati mwingi umepita) mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu, nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima , ambao akili zao, kwa kutumiwa,zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.” Mtume Paulo katika Iwakorintho 3:1-2 anawaambia Wakorintho,lakini ndugu zangu mimi sikuweza kusema nanyi kama watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini,kama na Watoto wachanga katika Kristo.Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza Naam, hata sasa hamkiwezi kwa maana hata sasa nini ni watu wa tabia ya mwilini,Basi wekeni mbali uovu wote na hali yote na unafiki na husuda na masingizio yote.Kama Watoto wachanga waliozaliwa kuukulia wokovu ,kiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye adhili (1 Petro 2:1-3) Wakati wa kasimamia vikundi hivi jumuiya na fellowships tuhakikishe kuwa vyote vinaamini katika kanisa moja takatifu ambalo ndilo Bwana wetu Yesu Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yake na kuwa Mchungaji mkuu ni Bwana wetu Yeu Kristo peke yake.Tuwe kundi moja chini ya mchunga mmoja tu bali roho ni yeye yule yaani Roho Mtakatifu.