• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
  • 24 Nov, 2023
  • Admin

Mwanzo 1:28-29

Mungu ameturuhusu vitu alivyoviumba viwe chakula chetu. Mungu akasema, Tazama nimewapa kila mche utaoa mbegu ulio juu ya uso wanchi yote pia,pia na kila mti, ambao matunda yake yenye mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu,” Pamoja na majani yote ya miche. Mwanzo 9:2-3 “Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani; pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu. Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.”

Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni, mkaongezeke mkaijaze nchi,na kuitiisha, mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” Nanyi zaeni, mkaongezeke, zaeni katika nchi, mkaongezeke ndani yake. Mambo Walawi 26:9 “Nami nitawaelekezea uso wangu, na kuwapa uzazi mwingi, na kuwaongeza, nami nitalithibitisha agano langu,pamoja nanyi.” Nami nitakwenda kati yenu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Neno la Mungu linatuonya kwamba siku za mwisho kutakuwa na roho zidanganyazo. 1 Timotheo 4:1-5 “Basi roho anena wazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani,wakisikiliza  roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamira zao wenyewe, wakiwazuia watu wasioe, na kuamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokelewa  kwa shukrani, kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.”

ROHO

 

Jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana . Malaki 2:15(b) “Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.” Huyu ni mke wa agano lako ukimtenda mambo ya hiana BWANA  hataiangalia dhabihu yako hata kama umetoa kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hataiangalia hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwako na kuiridhia (Malaki 2:13).

SERIKALI.

Ili kulinda na kutunza uumbaji wa Mungu serikali nyingi duniani zimeweka sera na sheria mbalimbali kama vile;sheria za bahari, sheria za ardhi, mazingira, misitu na sheria za kulinda wanyama pori na viumbe wengine wengi. Uwekaji wa sheria hizi ni jambo jema lakini jambo kubwa zaidi ni kuzingatia sheria na maagizo ya Mungu.

MACHUKIZO

Mambo ya Walawi 18:22-23 “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo wala usilale na mnyama yoyote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye ni uchafuko.” Kwani mtu awaye yote atakaefanya machukizo hayo moja wapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao. Katika kitabu hicho hicho cha Mambo ya Walawi 20:13,15-16 linasema, “Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa, damu yao itakuwa juu yao. Tena mtu mume akilala na mnyama,hakika atauawa; nanyi mutamwua huyo mnyama. Tena mwanamke akimkaribia mnyama yoyote na kulala pamoja naye, mtamwuwa huyo mwanamke, na mnyama pia.”  

 

UKAHABA

Kumbukumbu la Torati 23:17-18 “Pasiwe na kahaba katika binti za Israel, wala pasiwe na hanithi katika wana wa Israel wanaume. Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yoyote; kwani hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili.” Kuna vitu saba anavyovichukia  BWANA vilivyo chukizo kwake.

TOBA

Ezekieli 18:27-28 “Tena mtu mwovu atakapoghairi na kuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai. Kwa sababu atafakari na kughairi, na kuyaacha makosa yake yote aliyoyatenda, hakika ataishi, hatakufa.” Tupilieni mbali  nanyi makosa yenu yote mlioyakosa,jifanyieni moyo mpya na roho mpya. Bwana wetu Yesu Kristo anatufundisha kuwa lazima uzaliwe mara ya pili kwa maji na roho ili uwe kiumbe kipya na mtu wa Mungu aliye hai.

VITU SABA VILIVYO CHUKIZO.

Mithali 6:16-19 “Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; naam viko saba vilivyo chukizo kwake. Macho ya kiburi, ulimi wa uongo,na mikono imwagayo damu isiyo na hatia, moyo uwazao mawazo mabaya; miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; shahidi wa uongo asemaye uongo, naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.” Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu kwa njia ya toba.

HEKALU LA MUNGU.

I Wakorintho 6:19-20 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mlipewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” Warumi 12;1 “Basi ndugu zangu, na wasihi kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai takatifu ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Wala msifuatishe namna ya dunia hii na taama zake. I Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi. Neno hili linasisitizwa kwenye I Wakorintho 6:19-20 …………… I Petro 1:18-19 “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa babu zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani ya Kristo.” Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa  wa dhambi au watumwa wa wanadamu. Mtume Paulo anafundisha kuwa Kristo ataadhimishwa katika mwili wake ikiwa kwa maisha yake au ikiwa kwa mauti yake. Huu ni msimamo wenye nguvu kuhusu Bwana wetu Yesu Kristo  kwa maana anasema  kwake yeye kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.

I Wathesalonike 5:23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakasa kabisa, nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili bila lawama wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.”

UWAKILI

Wakili ni mtu aliyekabidhiwa mali ya mtu mwingine ailinde, aitunze na kuiongoza. Mungu ametukabidhi uumbaji wake ambao ni mali yake ili tuulinde, tuutunze na kuuongoza. Mwanzo 1:28 ……… “Jambo moja muhimu katika uwakili ni uaminifu, kwa hiyo tunatakiwa kuwa waaminifu kwa Mungu; kwani tutatoa hesabu siku Bwana na atakapo kuja. Tunawajibika kwake kwa matumizi sahihi ya uumbaji  yaani mbingu na nchi Zaburi 24:1 “Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, dunia na vitu vyote, vilivyomo ndani yake. I Wakorintho 4:1-2  Mtu na  atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena  inayo hitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.” Bwana wetu Yesu Kristo katika Luka 12:41-42 “Bwana akasema, ni nani basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?  Heri mtumwa yule ambaye  bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo.” Na kila aliyepewa vingi kwake huyu vitatakiwa vingi; naye waliye mwekea amana vitu vingi kwake huyo watataka zaidi. Mfano  mzuri ni ule wa mtu aliye weka mali zake kwa watumwa wake watatu. Watumwa wawili waliweza kuzalisha talanta zao lakikini watatu hawakuzalisha chochote. Akawaambia wale walio zalisha ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya Bwana wako. Yule ambaye hakuzalisha  akanyang’anywa hiyo talanta akapewa aliyenazo kumi. Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongozewa tele; lakini asiye na kitu hata kile alichonacho atanyang’anywa (Mathayo 25;14-29). Wakili mwema mwenye busara hulinda mali ya BWANA wake na kuendeleakuzalisha na kuzaa matunda mpaka BWANA wake atakapokuja. 

ZINAA.

Katika AganoJipya Mtume Paulo anafundisha kuwa Mungu aliwaacha katika tamaa zao wafuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao baada ya kuacha kumhimidi Muumba wao. Warumi 1:26-27 “Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili, wanaume nao vivyo hivyo waliacha matumizi ya mke, ya asili wakawakiana tamaa, wanaume wakayatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Kwa maana waasherati, wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti hawataurithi ufalme wa   Mungu (Warumi 6:9-10).

 

MWILI

Mwili ni ile sehemu ya mwanadamu ambayo BWANA Mungu alimfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi ambayo mtu akifa tunazika kama vile Mungu alivyosema ya kwamba u mavumbiwewe, nawe mavumbini utarudi.Hili ni gamba la nje la mwanadamu lenye viungo mbalimbali vinavyoonekana kwa macho ya kawaida au sehemu za ndani zinazoweza kuonekana kwa kutumia mionzi ya X-ray na aina zingine za mionzi.Huu ndio mwili ambao tunatakiwa kuulinda na kuutunza kwa kuwa ni hekalu la Mungu.

 

WARUMI 7:14-24.

Hekalu hili la Mungu yaani mwili wako linatakiwa kulindwa na kutunzwa kwa sababu ni dhaifu tena linavutiwa na tamaa za dunia hii ambazo huitwa tamaa za mwili.Waraka wa Mtume Paulo kwa Warumi 7:14-24 Paulo anafundisha kuwa mwili ni dhaifu ndio maana lile nilipendalo, silitendi.Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi, bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye.

Bali ile dhambi ikaayo ndani yangu, iliyo katika viungo vyangu.Ole wangu maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.Njia pekee ya kukwepa mauti ya dhambi ni kuyasafisha matendo ya mwili huu wa mauti kwa damu ya Mwana-kondoo wa Mungu kwa uongozi wa Roho Mtakatifu.

 Warumi 13:14 “Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake”.Kwa kuwa, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufuaYesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa roho wake anayekaa ndani yenu (Warumi 8:11) .Neema ya Mungu ituongoze tutubu dhambi zetu ili dhambi isitawale ndani ya miili yetu wala tusiendelee kuvitoa viungo vyetu kuwa silaha ya dhuluma kwa dhambi bali tujitoe wenyewe kwa Mungu ili  tuwe hai na viungo vyetu kuwa silaha za haki tupate kutakaswa na mwisho wake tupate uzima wa milele.

 

ROHO

Roho ni ile pumzi ya uhai ya Mungu aliyopulizia puani mwili wa mtu aliyemuumba, kutokana na mavumbi ya ardhi,mtu akawa nafsi hai. Pumzi hii yauhai yenye uzimaikimtoka mtu anakufa nayo pumzi humrudia Mungu aliyeitoa.Mhubiri 12:7 “Nayo mavumbi kurudia nchi kama yalivyokuwa,nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.” Maana mwili pasipo roho umekufa(Yakobo 2:26). Pumzi hii au roho  imehifadhiwa ndani ya moyo wa mtu ndio maana sehemu zingine maneno haya mawili (moyo/roho) yanatumika kwa pamoja. Kumbukumbu la Torati 6:5 “Nawe mpende BWANA, Mungu wako,kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote,na kwa nguvu zako zote”.

Roho ni sehemu ya mwanadamu yenye kumwezesha kumpenda Mungu na kutambua mambo ya Mungu au siri za Mungu.Kazi ya roho ndani ya mwanadamu ni pamoja na;

·       kumwabudu Mungu,

·       kupokea mafunuo kutoka kwa Mungu,

·        kupambanua roho, na

·       kupokea karama za Roho Mtakatifu na kutia mwili uzima

Hii ndiyo roho aliyoiumba Mungu ambayo tunatakiwa kuilinda na kuitunza ili imzalie tunda la roho.

 

ROHO ZIDANGANYAZO

Roho zidanganyazo nia yake ni mauti iletwayo na dhambi bali nia ya roho ni uzima na amani  katikaBwana wetu Yesu Kristo. Ezekiel sura ya 18 Neno la Mungu linasema kuwa roho itendayo dhambi itakufa bali kama mtu ni mwenye haki, na kuyatenda yaliyo halali na haki mbele za Mungu hakika ataishi, asema Bwana Mungu.Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo, lakini sasa mmerudia Mchungaji  na mwangalizi wa roho zenu (1Petro 2:25). Tumwombe Mungu kwa roho na kwa akili kwa ajili ya wokovu wetu. 2Timotheo 4; 22“Bwana na awe pamoja na roho yako.Neema na iwe pamoja nanyi.” Roho yako imfurahie Mungu, Mwokozi wakokwa kuwa jina lake ni takatifu.Mungu ni roho nao wamwabuduo yeye                                                                    inawapasa kumwabudu katika roho na kwelli (Yohana 4:24) nao watapata raha nafsini mwao. Tumwombe Mungu atupe ufunuo wa kupambanua roho na atupe karama za Roho Mtakatifu wake kulingana na mapenzi yake. Kazi ya karama ya kupambanua roho ni kugundua aina mbalimbali za roho takatifu au roho chafu na kuziweka hadharani kwa watu wote.

 

 

NAFSI

Katika maandiko yaliyopita tumejifunzza kuwa baada ya Mungu kumpulizia mtu pumzi yake akawa nafsi hai.Nafsi ni ile sehemu inayobeba vitu  vitatu;  akili, hisia na maamuzi (utashi) ya mtu.Nafsi inapata taarifa au ripoti kutoka milango mitano ya fahamu; macho, masikio, ngozi, pua na ulimi.Taarifa hizi zinapokelewa na kuchambuliwa kwenye akili alafu maamuzi hutolewa na hisia za maamuzi hayo zinaonekana kama vile furaha, huzuni, maumivu, kilio, kicheko, uchungu, aibu na kujuta. Ikiwa maamuzi mabaya  yamefanyika utajua kwa kuona hisia zake, ikiwa maamuzi mazuri yamefanyika utajua pia kwa hisia zinazojitokeza.Taarifa zinaweza kuwa zimebeba majaribu kama vile alipojaribiwa Eva /Hawa na shetani.Shetani akampa taarifa za udanganyifu  kuwa hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakapokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya .Katika kuchambua taarifa hii akilini mwake mwanamke (Eva/Hawa) akaona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa. Akafanya maamuzi akatwaa katika matunda  yake  akala, akampa na  mumewe (Adamu)_naye akala.Hisia zilizojitokeza zilikuwa mbaya, wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakaogopa wakajificha Mungu asiwaone.Pamoja na hukumu zingine wakahukumiwa kifo; Mungu akawaambia kwa maana u mavumbi wewe, na mavumbini utarudi (Mwanzo 3:1-10). Maamuzi yoyote yale yanayotokana na dhambi yanaleta uchungu, majuto, huzuni, iabu, kilio na hata kifo. Zaburi 49:20 “Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili, amefanana na wanyama wapoteao.” Mtu  akifanya maamuzi kutokana na hisia zake bila ya kufikiri vizuri ana hatari kubwa ya kufanya maamuzi ambayo sio mazuri yaani maamuzi mabaya.Bwana wetu Yesu Kristo alipojaribiwa mara tatu na shetani kule nyikani,alisikiliza taarifa au hoja za shetani kwa makini na kwa kuwa alikuwa na akili za ki-Mungu  alimjibu shetani sawa sawa na neno la Mungu naye akamshinda.Baada ya ushindi huo tazama wakaja malaika wakamtumikia (Mathayo 4:1-11).Ushindi  huo unatufundisha kuwa hata wewe ukitumia neno la Mungu kulingana na jaribu lililoko mbele yako utashinda. Ikiwa nafsi yako itaamua vyemaakilini mwako matokeo yake yatakuwa furaha, kicheko, amani na upendo. Hii ndiyo nafsi aliyoiumba Mungu ambayo tunatakiwa kuilindana kuitunza ili imhimidi Bwana.

KUTAKASA NAFSI

Ili nafsi yako imhimidi Bwana wala usije ukaiharibu nafsi yako huna budi kujitakasa kwa damu ya Mwana – Kondoo wa  Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu ambaye aliitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu.Yohana 10:11 “Mimi ndimi mchungaji mwema.Mchungaji mwema hutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo”.Ikiwa yeye alitoa nafsi yake  kwa ajili yetu na sisi hatuna budi  kutoa nafsi zetu kwa ajili yake.Bwana wetu Yesu Kristo  katika Mathayo 10:39 anasema, “Mwenye  kuiona nafsi yake ataipoteza naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.” Tunatakiwa kutoa maisha yetu kwa ajili ya kumtumikia Mungu kwa uaminifu.Unapoingia majaribuni isemeshe nafsi yako habari njema ya neno la Mungu na ahadi zake ili kushinda shambulizi lolote lile. Ukiisemesha nafsi yako namna hiyo utapata nguvu na ujasiri wa kukabiliana na jaribu lililoko mbele yako kwa kuwa imani yako kwa Mungu na Mwana wake wa pekee itaongezeka .Mfalme Daudi ni mfano mzuri wa watu waliokuwa na ufunuo wa kuisemesha nafsi yake.Daudi aliimba zaburi nyingi  za aina hii.Zaburi 62:1-2 “Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya, wokovu wangu hutoka kwake. Yeye tu ndiye mwamba wangu wa wokovu wangu, ngome yangu, sitatikisika sana.” Tumaini langu hutoka kwake na yeye ni kimbilio langu kwani wema na fadhili ziko mikononi mwake. Zaburi 103:1-2, 8, 13, 20-22. “Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Naam, vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu.Ee, nafsi yangu umhimidi BWANA, wala usizisahau fadhili zake  zote.Bwana amejaa huruma na neema, haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao.Mhimidini BWANA enyi Malaika zake, ninyi mlio hodari mtendao neno lake.Mkiisikiliza sauti ya neno lake.Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote, ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake.Mhimidini BWANA, enyi matendo yake  yote, mahali pote pa milki yake.Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.”

 

Share This