• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
service photo

                                                                                                                        14 June 2021

MAISHA YA  GRACE  MARKO  SHAIDI ( Mrs. MUNGWE)

Nilizaliwa tarehe 20/04/1958 katika kijiji cha Vudee,wilaya ya Same,nikiwa mtoto wa sita wa Bw/Bi Marko Chalambo Shaidi .Namshukuru sana Mungu kwa kunipa familia kubwa na iliyo jaa upendo  na furaha,Ninakumbuka utoto wangu kwa tabasamu .

Nilipata elimu ya msingi kwenye shule tofauti nne  ikiwemo Vudee Indini.kuhamahama huko kulitoka na na uhamisho wa kikazi wa baba yangu ambaye alikuwa mwalimu.Licha ya ugumu ulioambatana na kuhama huko ,nilipata muda mzuri sana wa kuishi na baba yangu na kuwa na mahusiano ya karibu naye

Mwaka 1973-1978 nilipata elimu ya sekondari  katika shule ya wasichana Msalato ( Dododma) na Korogwe (Tanga) .Bado nakumbuka siku niliyosafiri kwa mara ya kwanza nikitoka Kondoa kwenda Dodoma mjini peke yangu. Basi la abiria tulilosafiria liliharibika njiani na by the time tunafika maeneo ya Msalato ilikuwa ni usiku wa manane. Licha ya kusisitiza nishushwe kwenye kituo cha Msalato baadhi ya abiria walipinga na  kumkataza dereava kunishusha na wanafunzi wengine wawili ambao nao pia walikuwa wanakwenda kuanza kidato cha kwanza.Ndipo mama mmoja na mumewe  walipojitolea kuwa  watatupa malazi  nyuimbani kwao na asubuhi  yake watatupeleka mahali ambapo tutapata gari la shule. Miaka hiyo watoto hawakuwa  wa famiia yao tu bali waliangalia na jamii . There were good people . Namshukuru sana  Mungu  kwa ajili ya familia hiyo. Nakumbuka pia safari nyingi za treni  kati  ya Dodoma na Moshi  kupItia  Ruvu zilikuwa  safi ndefu na tulijazana  saana kwenye  vyumba vya treni  kwa sababu  shule  zilifungwa  kwa wakati  mmoja  wa  treni  ilikuwa ndiyo njia iliyotumiwa na Serikali kusafirisha  wanafunzi.

Nilijiunga na Jeshi la Kujenga  taifa (JKT)kituo cha Oljoro, Arusha  mwaka 1979. Itakumbukwa kuwa huo mwaka ndio Tanzania iliingia vitani na Uganda  chini ya Idd Amini. Vijana wengi wa kiume tulikuwa nao jeshini  walipelekwa  kutumika vitani. Haukuwa wakati mrahisi.

Nilihitimu shahada ya usanifu  majengo (Architecture) katika chuo cha Ardhi ,Dsm mwaka 1983 na kupangiwa kazi kituo cha Dodoma,Mamlaka ya ustawishaji  makao makuu (CDA) interestingly,nilisoma Dodoma na kurudi kufanya kazi Dodoma na baadae kuishi jirani kabisa na Msato .

 Niliolewa na kupata mtoto wangu wa kwanza mwaka 1985.

Nikiwa kazini nilipata nafasi ya kusoma Masters  nchini Ubeligiji  mwaka 1990 na nikatunukiwa shahada ya Architecture –Human Settlements.

Nikiwa Ubeligiji na familia yangu nilibarikiwa kupata mtoto wangu wa pili. Niliporudi nchini niliendelia kufanya kazi CDA  mpaka zoezi la kupunguza  wafanyakazi  lilipofanyika na mimi nikawa mmoja wa wale waliopunguzwa.  Bila kujua hii ikawa ni baraka kubwa kwangu kwani Mungu alifungua milango mingine.Mwaka 1997 nilipata nafasi ya kazi ya muda mfupi katika shirika  la umoja wa mataifa la kuhudumia  wakimbizi (UN Refugee Agency-UNHCR) .Mkataba  wa  mwezi  mmoja  nilioanza nao ukaendelea kuongezwa  kidogo kidogo na mwaka 2000 nikapewa mkataba  wa kudumu “indefinite contract” ingawaje kituo changu cha kazi kilikuwa Kigoma  na baadae Kibondo. Kazi yangu ilinipa nafasi kutembelea  na kutumika  katika makambi  yote ya wakimbizi  yaliyokuwa Kigoma  na Kagera  jumla  ya makambi kumi na moja . Kazi  kubwa  ilikuwa ni kutengeneza  michoro  ya makambi na majengo pamoja na  kusimamia utekelezaji  wake .Nilifurahia  kazi yangu na kuifanya kwa bidii  na uadilifu.Wakati wote nilimtegemea Mungu na mkono wake haukupunguka kwangu. Kwa mara  ya kwanza mwaka 2003 mwanzoni  niliomba kazi nje na nilichaguliwa kwenda Sierraleone. Mwaka hadi mwaka Mungu aliniinua kutoka ngazi moja hadi nyingine.  Nilifanya kazi katia nchi mbalimbali  mpaka  mwaka 2020 nilipostaafu. Ni mwaka mmoja sasa umetiamia.Muda niliofanya kazi  katika nchi ya Somalia umeacha kumbukumbu isiyosahaulika kwa urahisi moyoni mwangu.  Kipindi hicho nchi ilikuwa kwenye vita  na  athari (risks) za utekaji nyara  zilikuwa kubwa sana kazi yangu ilinihitaji kusafiri ndani ya nchi hiyo kutoka utawala mmoja kwenda mwingine na kwa hakika ni mkono wa Bwana ulionilinda wakati wote.

Nilipokaribia kustaafu nilidhamiria  moyoni mwangu  kuwa  Mungu  akinisaidia nimalize muda wangu wa ajira na kuweza kurudi nyumbani salama ,nitamtolea shukurani katika usharika wa Vudee .Ikumbukwe kuwa wakati huo ugonjwa wa COVID-19 ulishaanza na nilikaa kwenye qurantaine kwa miezi mitatu nikiwa India –kituo changu cha kazi cha mwisho .Isingekuwa kwa serikali ya Tanzania kutuma ndege yake India  kuwawazesha raia wake  waliokwama nchini india   kurudi nyumbani,ingechukuwa muda mrefu kupata jinsi ya kurudi Tanzania.Naishukuru sana serikali yangu .

Kwa neema ya Mungu mnamo tarehe 04/04/2021 nilipata kibali na kuweza kutimiza ahadi ya kumtolea  Mungu wangu shukurani .Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kwenda Vudee kwa ajili hiyo .Vilevile namshukuru sana Mungu kwa ajili ya ndugu zangu wote walionizingira na kushirikiana pamoja nami baraka hii .Hakika tuliuona mkono wa Bwana na tulipata muda mzuri wenye wingi wa furaha pamoja. Neno la shukrani lilitoka katika kitabu cha Zaburi 28:6-7 na Wimbo tuliouchagua ni kutoka  kitabu cha Mwimbieni Bwana namba 405,(Mbele ninaendelea).

Kipindi hiki baada ya kustaafu kinaendelea kuwa cha baraka sana na kinanipa muda wa kuwa  karibu na familia yangu  hasa watoto na wajukuu  zangu, lakini pia kushiriki katika shughuli za ukoo wangu.zaidi ya yote napata muda mzuri wa kumtumikia  Mungu kwa vitendo.

Ninamaliza kwa kuwashukuru sana mabinti zangu kwa uvumilivu wao katika kipindi chote ambacho nimekuwa nafanya kazi  mbalimbali

Jina la Bwana lihimidiwe Tangu leo na Hata Milele ,Zaburi  113 :2

Bofya hapa kupata picha na video za tukio hili- https://drive.google.com/drive/folders/1Pk3GUEKhxbGY80LOuAau7AF7RhnHijaH?usp=drive_link


Ndungu zangu wapendwa katika Bwana wetu Yesu Kristo.Nimefurahishwa sana na Grace kwa kuchagua fungu jema.Amechagua kumshukuru Mungu kwa kuwa ni mwema na fadhali zake ni za milele.Ameuona ukuu na uweza wa Mungu katika maisha yake.Twendeni Vudee tuungane naye kumtolea Mungu sadaka za shukrani kwa kuwa amejaa utukufu, heshima na adhama ni mwingi wa rehema na sio mwepesi wa hasira.Siku hiyo tutatoa pia ile sadaka tuliyotoa siku ya kikao cha Marko's kilichofanyika nyumbani kwake.Tutaimbaje wimbo mpya ugenini? Zaburi 137:4 "Tuuimbeje wimbo wa BWANA katika nchi ya ugeni ? Karibuni nyumbani Vudee tusimulie mate ndo makuu ya Mungu aliyotutendea katika maisha yetu.Mungu alibariki tendo hili na azitakabali sadaka zetu.

Ndugu zangu, 

Ninawasalimuni wote katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Ninaandika message hii kwa moyo wa unyenyekevu sana nikimshukuru Mungu kwa baraka zake kwetu.  Tendo la kumtolea Bwana  shukrani tarehe 4 April 2021 lilienda vizuri sana chini ya mkono wake wenye nguvu. Tulikuwa na vipindi vizuri vya  kujifunza neno la Mungu, kuomba, kuimba na kusifu.  As a family, tulipata pia muda mzuri wa kuwa pamoja na kufurahi.

Basi ninawaomba wote mpokee shukrani zangu kwenu kwa upendo na ushiriki wenu katika kutimiza kusudi la moyo wangu na nadhiri niliyokuwa nimeiweka mbele za Mungu.  Nilifurahi sana kusimama madhabahuni pa Mungu nikiwa nimezungukwa na ndugu zangu na kujua kuwa hata wale walioshindwa kuja Vudee walisimama nami katika maombi na shukrani. Asanteni sana. 

Wifi Marge na kaka Vince walinifanyia surprise ya cake. It was indeed a surprise. Asanteni. 

Eddy na Rachel, ninawashukuru sana kwa kujitoa kubakia Vudee wakati wengine tulipoondoka ili kuiweka nyumba yetu...Holiday Home kwenye hali nzuri ya usafi. Ninawashukuruni sana.

Basi, Mungu mwenyewe atubariki sisi na vizazi vyetu. Tuzidi kupendana, kusaidiana na kuombeana katika mambo yote. UPENDO ni amri ya Mungu kwetu.

I can't thank you enough.

Nahavacheni mno.