KUSIMIKA KIONGOZI WA FAMILIA
KULINGANA NA NENO LA MUNGU.
Kiongozi wa familia anayo majukumu mengi na ili aweze kutekeleza wajibu wake ipasavyo anatakiwa;
Ãâ÷ Kiongozi amtumaini na kumtegemea Mungu,
Ãâ÷ Kiongozi awe hodari na shujaa,
Ãâ÷ Kiongozi awe na silaha za kivita,
Ãâ÷ Kiongozi atawale kwa haki bila ya upendeleo,
Ãâ÷ Kiongozi awe na upendo,
Ãâ÷ Maombi na maombezi.
Kiongozi amtumaini na amtegemee Mungu
Zaburi 27: 1-4,
Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu,nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia wanile nyama yangu, watesi wangu na adui zangu, walijikwaa wakaanguka. Jeshi linapojipanga kupingana nami, moyo wangu hautaogopa.Vita vijaponitokea hata hapo nitatumaini. Neno moja nimelitaka kwa BWANA, nalo ndilo nitakalolifuata; nikae nyumbani mwa BWANA siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa BWANA nakutafakari hekaluni mwake.
Zaburi 37:3-5
Umtumaini BWANA ukatenda mema, ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu. Nawe utajifurahisha kwa BWANA, naye atakupa haja za moyo wako. Umkabidhid BWANA njia yako, pia umtumaini naye atafanya.
Zaburi 46:1-2,11,
Mungu kwetu ni kimbilio na nguvu. Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
Zaburi 91:2,
Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
Yeremia 15:20-21,
Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa, nao watapigana nawe, lakini hawatakushinda, maana mimi nipo pamoja nawe ili nikuokoe na kukuponya, asema BWANA, nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha.
Yeremia 16:19-21,
Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yatatoka ncha za dunia, wakisema, Baba zetu hawakurithi kitu ila uongo, naam ubatili na vitu visivyofaa. Je, mwanadamu ajifanyie miungu, wasio miungu? Basi, tazama, nitawajulisha mara moja hii nitawajulisha, mkono wangu na nguvu zangu, nao watajua kuwa jina langu ni YEHOVA.
Yeremia 17:5-8,
BWANA asema hivi amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni mwake amemwacha BWANA. Maana atakuwa kama fukara nyikani hataona yatakapotokea mema, bali atakaa jangwani palipo ukame, katika nchi ya chumvi, isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, ambaye BWANA nitumaini lake maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, uenezao mizizi yake karibu na mto, hautaona hofu wakati wa hari ujapo, bali jani lake litakuwa bichi; wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha kuzaa matunda.
Yeremia 33:3,
Niite nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.
Isaya 42:6-10,
Mimi, BWANA nimekuita katika haki nami nitakushika mkono na kukulinda na kukutoa uwe agano la watu na nuru ya mataifa, kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa. Mimi ni BWANA ndilo jina langu na utukufu wangu sitampa mwingine wala sitampa sanamu sifa zangu. Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri mambo mapya, kabla hayajatokea nawapasheni habari zake. Mwimbieni BWANA wimbo mpya na sifa zake tokea mwisho wa dunia.
I Timotheo 6:17,
Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune,wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumainie Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.
Kiongozi awe hodari na shujaa.
Neno la Mungu linaweza kusomwa kutoka katika maandiko matakatifu yafuatayo:-
Kumbukumbu la Torati 31:6
Iweni hodari na moyo wa ushujaa, usiogope wala msihofu kwa maana BWANA, Mungu wako yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe hatakupungukia wala kukuacha.
Yoshua 1:9
Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa, usiogope wala usifadhaike, kwa kuwa BWANA, Mungu wako yu pamoja nawe kila uendako.
Yoshua 10:25
Yoshua akawaambia msiche, wala msifadhaike, iweni hodari na mioyo ya ushujaa, kwa kuwa ndivyo BWANA atakavyowafanyia adui zenu wote ambao mwapigana nao.
Yeremia 1:8
Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA.
I Wakorintho 16:13
Kesheni, simameni imara katika imani, fanyeni kiume, mkawe hodari.
Zaburi 31:24
Iweni hodari, mpige moyo konde, ninyi nyote mnaomngojea BWANA.
2 Timotheo 1:7
Maana Mungu hakutupa roho ya woga bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Kiongozi awe na silaha za kivita.
Waefeso 6:10-18
Hatimaye mzidi kuwa hodari katika BWANA na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweze kuzipinga hila za Shetani kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, namkiisha kuyatimiza yote, kusimame. Basi simameni hali mmejifunga kweli viuno, na kuvaa dirii ya haki kifuani na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya amani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, Mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.
2 Wakorintho 10:3-5
Maana ingawa tunaenda katika mwili hatufanyi vitu kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome); tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na kukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatiliza, maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia.
2 Wakorintho 6:7
Katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto.
1 Petro 4:1-2
Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ileile kwa maana yeye aliteswa katika mwili ameachana na dhambi. Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, wa kukaa bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki.
Kiongozi atawale kwa haki bila ya upendeleo
Mwanzo 6:9,
Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake. Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.
Mambo ya Malawi 19:15,
Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.
Kumbukumbu la Torati 10:17-18
Kwa maana BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa.
Wafalme 3:9
Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili ni wahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya, maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi.
Zaburi 11:7
Kwa kuwa BWANA ndiye mwenye haki, apenda matendo ya haki, wanyofu wa moyo watamwona uso wake.
Zaburi 17:1-2
Ee BWANA, usikie haki, ukisikilize kilio changu, utege sikio lako kwa maombi yangu, yasiyotoka katika midomo ya hila. Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yatazame mambo ya adili.
Zaburi 34:15
Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, na masikio yake hukielekea kilio chao.
Zaburi 37:25 âââ‰â¬Å 31
Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, lakini sijamwona mwenye haki ameachwa wala mzao wake akiomba chakula. Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, na mzao wake hubarikiwa. Jiepue na uovu, utende mema, na kukaa hata milele. Kwa kuwa BWANA hupenda haki wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, bali mzao wa wasio haki ataharibiwa.
Wenye haki watairidhi nchi, nao watakaa humo milele. Kinywa cha mwenye haki hunena hekima, naulimi wake husema hukumu. Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake. Hatua zake hazitelezi.
Zaburi 68:3
Bali wenye haki hufurahi, na kuushangilia uso wa Mungu; Naam, hupiga kelele kwa furaha.
Mithali 2:9
Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, na adili, na kila njia njema. Maana hekima itaingia moyoni mwako, na maarifa yatakupendeza nafsi yako. Busara itakulinda, ufahamu utakuhifadhi.
Mithali 10:16,30-32
Kazi yake mwenye haki huuelekea uzima, mazao ya wabaya huuelekea dhambi. Mwenye haki hataondolewa milele bali wasio hawatakaa katika nchi. Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima, bali ulimi wa ukaidi utakatiliwa mbali. Midomo ya mwenye haki huyajua yatakayokubaliwa;bali kinywa chao wasio haki hunena ukaidi.
Mithali 14:34-35
Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu ya watu wote. Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara, bali ghadhabu yake itakuwa juu yake aletaye aibu.
Mithali 16:31-33
Kichwa chenye mvi ni taji ya utukufu, kama kikionekana katika njia ya haki. Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji. Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; lakini hukumu zake zote ni za BWANA.
Mithali 29:1-2
Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafula, wala hapati dawa. Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua.
Sefania 2:3
Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake, itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu, huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Mungu.
Mathayo 7:15
Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa. Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii. Au utamwambiaje nduguyo, niache nikitoe kibanzi katika jicho lako, na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Mathayo 25:45-46
Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, kadri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Matendo ya Mitume 10:34-35
Petro akafumbua kinywa chake, akasema hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo, bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.
Matendo ya Mitume 20:28
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha Kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Warumi 1: 17-18
Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata imani, kama ilivyoandikwa, mwenye haki ataishi kwa imani. Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
Wagalatia 2:16
Hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria, maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.
Waefeso 6:8
Mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru. Nanyi, akina bwana, watendeeni wao yayo hayo, mkiacha kuwaogofya, huku mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo.
Wakolosai 3:25
Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.
1 Wathesalonike 2:7-8,11-12
Bali tukiwa wapole katikati yenu,kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mweyewe. Vivyo hivyo nasi tukiwatumainia kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu. Vilevile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia, ili mwenende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.
1 Timotheo 5:17
Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.
1 Timotheo 5:20-21
Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope. Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele ya malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka, usifanye neno lolote kwa upendeleo.
Petro 5:2-4
Lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kujifanya vielelezo kwa lile kundi. Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtapokea taji ya utukufu ile isiyokauka.
Ufunuo wa Yohana 22:11-13
Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho,wa kwanza na wa mwisho.
Kiongozi awe na upendo
Mathayo 5:43-48
Mmesikia kwamba imenenwa ,umpende jirani yako, na umchukie adui yako,lakini mimi nawambia wapendeni adui zenu,waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni , maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki,Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani?Hata watoza ushuru. Je; nao hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa ,Je nao hawafanyi kama hayo?Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu .
Yohana 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe pekee,ili kila mtu amwaminiye asipotee ,bali awe na uzima wa milele .
Yohana 13:34-35
Amri mpya nawapa,mpendane kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo .Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.
Yohana 15:9-14
Kama vile Baba alivyonipenda mimi,nami nilivyowapenda ninyi kaeni katika pendo langu . mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu;kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake,Haya nimewaambia ili furaha yangu iwe ndani yenu na furaha yenu itimizwe.Amri yangu ndiyo hii, mpendane kama nilivyowapenda ninyi.Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.Ninyi mmekuwa rafiki zangu mkitenda niwaamruyo.
Warumi 5:8-9
Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi,kwa kuwa Kriso alikufa kwa ajili yetu,tulipokuwa tungali wenye dhambi .Basi zaidi sana tukisha kuhesabiwa haki katika damu yake tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
Warumi 12:9-11
Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu mkiambatana na lililo jema kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu.
Warumi 13:8-10
Msiwiwe na mtu chochote isipokuwa kupendana, kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue,Usiibe,Usitamani, na ikiwapo amri nyingine yoyote inajumlishwa katika neno hili ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.
1Wakorintho 13:1-8,13
Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika kama sina upendo nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.Tena nijapokuwa na unabii na kujua siri zote na maarifa yote nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima,kama sina upendo si kitu mimi.Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini,tena nikijitoa mwili wangu niungue moto,kama sina upendo hainifaidi kitu .Upendo huvumilia, hufadhili, upendo hauhusudu,upendo hautakabari,haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu hauhesabu mabaya, haufurahii udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote, huamini yote,hutumaini yote, hustahimili yote .Upendo haupungui neno wakati wowote, bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha zitakoma, yakiwepo maarifa yatabatilika. Basi sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
1Wakorintho 14:1
Ufuateni upendo na kutaka sana karama za rohoni ,lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.
1Wakorintho 16:13-14
Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume ,mkawe hodari.Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.
Wagalatia 5;13-15
Maana ninyi ,ndugu ,mliitwa mpate uhuru,lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo Maana torati yote imetimilika katika neno moja nalo ni hili; Umpende jirani yako kama nafsi yako. Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana.
Wakolosai 3:14-17
Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo ,ndio kifungo cha ukamilifu. Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja;tena iweni watu wa shukrani. Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo na tenzi za rohoni. Huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo ,fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
1Wathesalonika 4:9-10
Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie,maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana. Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi ndugu, mzidi sana.
1Timotheo 1:5
Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema na imani isiyo na unafiki.
1Timotheo 5:8
Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
2Timotheo 1:7
Maana Mungu hakutupa roho ya woga bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
2Timotheo 2:24-26
Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi, bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha ,mvumilivu,akiwaonya kwa upole wao washindanao naye,ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli wapate tena fahamu zao na kutoka katika mtego wa Ibilisi ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake.
Waebrania 10:24-25
Tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri, wala tusiache kukusanyika pamoja ,kama ilivyo desturi ya wengine,bali tuonyane na kuzidi kufanya hivyo kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Waebrania 13:1-2
Upendano wa ndugu na udumu. Msisahau kuwafadhili wageni , maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua .Wakumbukeni hao waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; na hao wanaodhulumiwa, kwa vile ninyi nanyi mlivyo katika mwili.
1Petro 4:8-11
Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. Mkaribishane ninyi kwa ninyi pasipo kunungâââ‰â¢unika . Kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama ,itumieni kwa kuhudumiana,kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. Mtu akisema na aseme kama mausia ya Mungu ,mtu akihudumu na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele Amina.
2Petro 1:7-8
Na katika utauwa wenu upendano wa ndugu na katika upendano wa ndugu, upendo.Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele,yawafanye ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
1Yohana 5:1-3
Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.Kwa maana huku ndipo kumpenda Mungu,kwamba tuzishike amri zake;wala amri zake si nzito.
2Yohana 1:5-6
Na sasa mama nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo,kwamba tupendane. Na huu ndio upendo tuenende kwa kuzifuata amri zake . Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.
Yuda 1:21
Jilindeni katika upendo wa Mungu ,huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo hata mpate uzima wa milele.Wahurumieni wengine walio shaka na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.
Maombi na Maombezi kwa ajili ya kiongozi anayesimikwa
Neno la Mungu linatutaka kufanya maombi na maombezi kwa ajili ya watu wengine, viongozi wa jamii, wasiookolewa, wakristo wenzetu, kanisa na wahudumu wake. Katika jambo hili maombi na maombezi yafanyike kulingana na jinsi roho wa Mungu atakavyowaongoza viongozi wa ibada.
1Timotheo 2:1.
Basi kabla ya mambo yote nataka dua, na sala, na maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote, kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka , tuishi maisha ya utulivu na amani katika utauwa wote na ustahivu .Hili ni zuri nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu , ambaye hutaka watu wote waokolewe na kupata kujua yaliyo kweli.
Waefeso 6:17-18.
Tena ipokeeni chapeo ya wokovu,na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu ;kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho ,mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.
Mwanzo 24:12.
Naye akasema,Ee Bwana,Mungu wa bwana wangu Ibrahimu nakuomba mambo yangu uyajalie yawe heri leo,ukamfadhili bwana wangu Ibrahimu.
Mwanzo 25:21.
Isaka akamuomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa.Naye BWANA akamwitikia na Rebeka mkewe akachukua mimba.
1Samweli 12:23-25.
Walakini mimi, hasha nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi, lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema na kunyoka .Mcheni BWAN tu mkamtumikie kwa kweli kwa mioyo yenu yote, maana kumbukeni jinsi alivyowatendea mambo makuu.Lakini kama mkiendelea kutenda mabaya ,mtaangamia , ninyi na mfalme wenu pia.
Mathayo 19:13-15.
Ndipo akaletewa watoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombea, wanafunzi wake wakawakemea. Lakini Yesu akasema, waacheni watoto wadogo waje kwangu wala msiwazuie, kwa maana walio mfano wa hao ufalme wa mbinguni ni wao .Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko.
Luka 1:13.
Lakini yule malaika akamwambia usiogope Zakaria maana dua yako imesikika na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume na jina lake utamwita Yohana.
Luka 22:31-32.
Akasema Simoni, Simoni tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike, nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.
Luka 23:34.
Yesu Kristo anatufundisha kuwaombea watu wengine kama alivyofanya pale msalabani aliposema Baba uwasamehe kwa kuwa hawajui watendalo.
Yohana 14:13-17.
Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana .Mkiomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya, Mkinipenda mtazishika amri zangu .Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea kwa kuwa haumwoni wala haumtambui bali ninyi mnamtambua ,maana anakaa kwenu naye atakuwa ndani yenu.
Yohana 17:9-10, 15-21.
Mimi nawaombea hao,siuombei ulimwengu bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako na wote walio wangu ni wako,na walio wako ni wangu, nami nimetukuzwa ndani yao. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndiyo kweli. Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe Baba ulivyo ndani yangu , nami ndani yako hao nao wawe ndani yetu , ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
Matendo ya Mitume 12:5
Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. Hata Petro alipopata fahamu akasema, sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi.
Matendo ya Mitume 14:23.
Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa na kuomba pamoja na kufunga wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.
Warumi 8:26-27.
Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo ,lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
Warumi 10:1-2.
Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu ni kwa ajili yao ili waokolewe. Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.
Warumi 15:30-33.
Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu, kwamba niokolewe na wale wasioamini katika Uyahudi, na tena huduma yangu niliyo nayo huko Yerusalem, ikubalike kwa watakatifu, nipate kufika kwenu kwa furaha, kama apendavyo Mungu , nikapate kupumzika pamoja nanyi. Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amina.
Wakolosai 4:2-4.
Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani , mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa ili niidhihirishe kama inipasavyo kunena.
1Wathesalonike 5:25-27.
Ndugu, tuombeeni wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu. Nawaapisha kwa Bwana, ndugu wote wasomewe waraka huu .Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.
2Wathesalonike 1:1-2, 11-12.
Paulo na Silwano na Timotheo kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo. Kwa hiyo twawaombea ninyi siku zote, ili Mungu wetu awahesabu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu; Jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo
Wathesalonike 3:1-2,
Hatimaye ndugu tuombeeni neno la Bwana liendelee na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu, tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani.
Tuhitimishe sehemu hii ya kuwaombea viongozi wanaosimikwa kwa kuwaasa kwa maneno haya. Jitunze nafsi yako na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia. Tuseme kwa pamoja maneno haya;
Mbarikiwa ni wewe Bwana Mungu wetu uliyeziumba mbingu na nchi, Mungu wa milele, unayeishi katika vizazi vyote. Wewe ni asili ya hekima takatifu na chemchemi ya ukweli.
Tunakushukuru kwa ajili ya viongozi wa aina mbalimbali miongoni mwetu wenye mfano wa kuigwa kwa maisha na utendaji wao. Tuwezeshe kufuata mfano wao tunapokutumikia kwa utayari na umoja wa moyo. Kwa Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wetu. Ameni.
Picha hizi zinaonyesha Joseph Heriel Ghuheni Shaidi akiwa anasimikwa kuwa kiongozi wa familia ya Herial Ghuheni Shaidi mnano tarehe 07/08/2016