Kulingana na matukio yaliyofanyika, sherehe za kifamilia za Krismasi zilianza tarehe 21 Desemba 2024 kwa ibada ya jioni iliyoanza saa 11:00 jioni katika kanisa la Vudee. Ibada hiyo iliendeshwa kwa mada kuu kutoka Kutoka 15:2, "BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu." Wimbo wa siku ulikuwa Namba 256 kutoka kwenye kitabu cha Tumwabudu Mungu Wetu, unaosema, "Njooni tumsifuni Mungu aliye Mwenyezi." Washiriki walihamasishwa kufika mapema ili kushiriki kikamilifu katika ibada hiyo ya kiroho na sifa.
Tarehe 22 Desemba 2024, baada ya ibada kanisani, familia ilikusanyika katika Vudee Holiday Home kwa hafla ya kumshukuru Mungu na kusherehekea mchango wa Edna Marko Mtanga. Hafla hiyo ilijawa na furaha na shukrani kwa huduma yake ya kuwalea na kuwatunza wazazi wake pamoja na familia kwa ujumla. Katika sherehe hizo, mgeni rasmi, Mrs. J.J. Mtanga, alipewa maua, zawadi mbalimbali kama dhahabu, fedha, mavazi, na keki ya shukrani kwa huduma yake ya upendo na kujitolea. Hafla hiyo ilifungwa kwa mgeni rasmi kutoa neno la baraka kwa familia, huku shukrani na sifa zikirudishwa kwa Mungu.
Usiku wa tarehe 24 Desemba 2024, familia iliadhimisha ibada ya Usiku Mtakatifu. Wajukuu na vitukuu walipangwa vizuri na walitoa mistari ya Biblia inayohusu kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo, jambo lililoleta hisia za kipekee na ukumbusho wa maana ya Krismasi. Mistari hiyo ilionyesha maandalizi mazuri ya walezi na watoto, na kushuhudia sherehe iliyojaa mshikamano wa kifamilia na heshima kwa Mungu.
Kwa ujumla, sherehe hizi ziliadhimishwa kwa furaha, mshikamano wa kifamilia, na kumsifu Mungu kwa matendo yake makuu, huku kila tukio likitimiza malengo yake kwa mafanikio makubwa.
Picha za matukio ya december 2024 zinapatikana kwenye link hii- https://drive.google.com/drive/folders/1yHqnah6OrAimEpvkXW-D8XM4qKQPEy-5?usp=drive_link
NENO LA KUONGOZA SHUKRANI ZETU LINAPATIKANA HAPA CHINI
SHUKRANI ZETU KWA MUNGU.
Kama familia moja ya Mungu wote tutamshukuru Mungu kwa ndimi za kelele za furaha na shangwe zilizojaa kicheko kwa kuwa BWANA ametutendea matendo makuu mengi na ya ajabu. Tukumbuke shukrani zinatupa ukaribu na Mungu kila siku na kila wakati. Tuanze kumshukuru Mungu kuanzia sasa na katika ibada ya tarehe 21/12/2024 na 22/12/2024 tutamshukuru Mungu kwa pamoja. Tumshukuru Mungu kwa mioyo yetu yote, kwa unyenyekevu na upendo wake kwetu tukikumbuka pamoja na haya yafuatayo:-
1. Tunamshukuru Mungu kwa kutupa wazazi ambao wametulea katika njia nzuri ya kumjua na kumpenda Mungu.
2. Tunamshukuru Mungu kwa mafanikio katika elimu na uchumi.
3. Tunamshukuru Mungu kwa kuzidisha uzao wetu na kuulinda.
4. Tunamshukuru Mungu kwa kutuokoa na watu wasio haki, wabaya, wasio na Imani.
5. Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya wazaliwa wetu wa kwanza pamoja na zawadi ya watoto wote aliotupa.
6. Tunamshukuru Mungu kwa wema wake na fadhili zake nyingi kwetu.
MAOMBI YETU KWA MUNGU.
Pamoja na shukrani zetu kwa Mungu tutapeleka haya za mioyo yetu. Tuanze kumwomba Mungu tangu leo hii hadi kilele cha shukrani zetu. Kila mmoja wetu amwombe Mungu haya ya moyo wake pamoja na haya yafuatayo ambayo tutayaomba kwa pamoja:
1. Tunamwomba Mungu uzao wetu uwe mzao mteule kwake na umiliki mlango wa adui.(1 Petro 2:9 (a) na Tito 2:14). Kenneth Shaidi
2. Tunamwomba Mungu atujalie maisha marefu yenye kumcha BWANA. Tuombe neema ya wokovu ( Mithali 10:27). Grace Shaidi
3. Tunamwomba Mungu awabariki wazaliwa wetu wa kwanza na watoto wetu wote ( Kutoka 13:12 na Luka 2:22-24). Vincent Shaidi
4. Tunamwomba Mungu ndoa takatifu kwa ajili ya vijana wetu wa kiume na wa kike. Ndoa zitakazofungwa na Mungu mwenyewe. ( Marko 10:9) Kenneth Shaidi.
5. Tunamwomba Mungu upendo wa ndugu na umoja udumu kati yetu. Tusigombane njiani (Yohana 13:34 na Petro 1:7). Leah Mwakyusa
6. Tunamwomba Mungu abariki uzao wetu kiuchumi,kiustawi na mafanikio katika maisha. Rachel Shaidi.