NENO LA SHUKRANI KWA WAZAZI WETU SIKU YA SHAIDI DAY ILIOFANYIKA TAREHE 06/04/2019 NYUMBANI KWA WILFRED A. SHAIDI.
Tunapenda kutoa shukrani za dhati kutoka mioyono mwetu kwa wazazi wetu wakina baba, mama,shangazi na wajomba zetu kwa malezi mazuri mliotupatia kiroho, kiellimu, kiuchumi, kijamii na msisitizo wenu mkubwa katika kuimarisha undugu huu. Tunaaini kuwa kama msingesimama imara baadhi yetu tusingekuwa hapa tulipo sasa.
Tunashukuru kwa juhudi za dhati kabisa ambazo zilifanywa na babu zetu nanyi mkaweza kuziendeleza kwa kuhakikisha kuwa mmeuweka ukoo pamoja. kwa kutambua kazi hii nzuri mliyo ifanya na mnaendelea kuisimamia tunaomba Mwenyezi Mungu awabariki sana.
Tunafahamu pia changamoto zilizoko sasa za kutuweka pamoja ni kubwa kushinda ilivyokuwa mwanzo kwa sababu zifuatazo:
ÃUkoo umepanuka sana kwa sababu wako ndugu ambao wameoa na kuolewa sehemu mbalimbali za nchi
ÃWanaokoo pia wanaishi maeneo mbali ya nchi kwa sababu mbalimbali za kimaisha.
Kutokana na sababu hizo hapo juu, wakati huu ndio wakati tunahitaji kushikamana na kushirikiana zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali. Mungu azidi kutuimarisha kiroho ili kila mmoja wetu aweze kutambua nafasi yake katika familia hii. Lengo la kila mmoja wetu liwe kuhakikisha kuwa umoja huu unaimarika.
Hivyo basi wapendwa baba, mama, shangazi, na wajomba zetu ili ukoo wetu uendelee kuimarika tunaomba kwa heshima mpokee mapendekezo yetu ambayo tumetoa ili na sisi kizazi chetu kiweze kuwa enzi wazee wetu kwa kuweka ukoo pamoja hadi na sisi tukapokabidhi kwa watoto wetu ikiwa shaidi moja ambayo haijameguka, na mapendekezo yetu yatawasilishwa kwenu kama ifuatavyo:
MAPENDEKEZO: WASEMAJI:
1:KUWE NA UWIANO SAWA KATIKA USHIRIKI WA MATUKIO -MRS ANNA NGOO
2: UPENDO USIO NA UBAGUZI -MRS JENIFER ITOSI
3:KUWA NA UTARATIBU MZURI WA KUENDESHA VIKAO -MR KILONZO MCHOME
4:KUWE NA UTARATIBU MZURI WA KUPEANA TAARIFA (WAZEE VS VITUKUU) -MRS NELLY LYARUU
Picha za tukio hili zinapatikana kwa kubofya hapa- Shaidi Day 2019