• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
service photo

TAARIFA FUPI YA KUMALIZA MSIBA WA BIBI WALEI ABRAHAMU SHAIDI (MLALA NAKADORI)

Ukoo wa Shaidi umejiwekea taratibu za kufuata wakati msiba unapotokea na hata pale ambapo shughuli ya kumaliza msiba inapofanyika. Taratibu zote huzingatiwa kipindi chote tokea msiba unapotokea hadi shughulia ya kumaliza msiba inapofanyika. Kiongozi wa Ukoo huratibisha shughuli yote kwa kushirikiana na ndugu wote, majirani na marafiki. Aidha, kamati mbalimbali huundwa ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanatekelezwa ipasavyo.

Mara baada ya kupata taarifa za msiba wa Mama na bibi yetu mpenzi Waeli Abrahamu Shaidi tarehe….. Kikao cha ukoo kilikaa nyumbani kwa Ndg Wilfred Abraham Shaidi tarehe ……….na kuteua kamati tendaji ya kuratibisha shughuli zote za mazishi na hatimaye shughuli ya kumaliza msiba. Kamati hiyo iliongozwa na Ndg Exaud Marko Shaidi aliyekuwa Mwenyekiti, Keneth Marko Shaidi (Katibu) na Anna Godwin Ngoo (Mhazini).

Shughuli ya kumaliza msiba wa Mama/Bibi ilifanyika tarehe 31 Machi, 2018. Shughuli hiyo ilitanguliwa na vikao vya maandalizi vitatu (3) vilivyofanyika katika Hoteli ya Shengena Manzese ili kujianda na kuhakikisha shughuli inafanyika vizuri na kwa heshima zote. Katika Kikao cha kwanza cha tarehe……. kilikubali rasimu ya bajeti ya shilingi 5,500,000 kwa ajili ya shughuli nzima. Bajeti hii ilipangwa kwa ajili ya Chakula kwa siku mbili, Usafiri na Sadaka ya shukrani iliyojitokeza katika kikao cha pili cha tarehe…….. Vyanzo vya mapato vya kukidhi bajeti hii ilitokana na kiasi cha fedha kilichobaki katika shuguli ya mazishi pamoja na michango ya wanafamilia. Kulingana na taratibu za ukoo wa Shaidi shughuli ya kumaliza msiba wa mama hufanywa na watoto wa kiume, hivyo watoto wote walipaswa kuchangia shilingi 100,000 na vitukuu kwa ujumla wao waliombwa kuchangia shilingi 50,000 kila mmoja.

Kikao cha 3 kilichofanyika tarehe…….., kilitathmini hali halisi ya michango na mipangilio ya shughuli na kubaini kuwa malengo yatafikiwa na hivyo kuruhusu kamati tendaji kuendelea na utekelezaji. Mambo ambayo yaliratibishwa na Kamati tendaji ni kama ifuatavyo:

Usafiri : Iliazimiwa kuwa safari ianze saa 1 asubuhi Shengena na njia ilipangwa kupitia Bagamoyo. Ndg Abraha Wilfred Shaidi na Ndg Kilonzo Exaud Shaidi walipewa majukumu ya kuratibu usafiri. Ndugu wa Mbeya na Chalinze walichuliwa Msata.

Safari ilianza kwa wakati kama ilivyopangwa pamoja na changamoto za kusubiriana hasa pale Mbezi, tulipata kifungua kinywa pale (group Picha)……... Aidha, kwa kuwa kulikuwa na mvua zinazoendelea kunyesha tulikutana na changamoto nyingine ya kukatika kwa daraja mara baada ya kuvuka Makanya. Ililazimu watu kushuka ktk gari na kusaidia kusukuma gari kama inavyoonekana katika picha ( Insert picha). Aidha, gari ilipofika milimani barabara ilikuwa imeharibika kwa kiasi kikubwa

kutokana na mvua zilizokuwa zikiendelea na kusababisha gari kukwama eneo linaloitwa……..,. Hapa watu wazima karibia wote, akina baba , mama, dada, na watoto walianza kutembea taratibu mpaka wakafika maeneo ambayo walipata usafiri mbadala na kuwafikisha nyumbani. Hatimaye ilitumwa gari aina ya Fuso na kwenda kukwamua gari lililokuwa limekwama. Safari ya kurudi ilikuwa shwari kwani usafiri haukusumbua popote ila Dreva alishangaa ali[pofika Korogwe…katika buti alikuta kuna vitukuu waliweka kondoo hai wanampekeka Dar bila kumwambia. Alishangaa jinsi vijana wa ukoo huu wanavyopenda nyama. Kondoo huyu alinunuliwa katika mnada pale kanisani siku ya jumapili mara baada ya ibada ya Pasaka.

Ibada: Ibada ya kumaliza msiba ilifanyika siku ya jumamosi tarehe 31 Machi, 2018 nyumbani Chome Muze. Ibada ilianza saa 5.30 asubuhi na iliongozwa na Askofu….., Mch. Msangi akisaidiwa na Msaidizi wa Askofu Mch. Ibrahim Ndekie, Mch. Kirumbiwa wa Usharika wa Chome na mch. Mstaafu.

Mahubiri yalitoka katika Injili ya Yohana 12: 20-12 “Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu. Basi aho walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu” katika mahubiri ilisisitizwa kuwa ninanukuu “..kila mtu katika Pasaka hii unatakiwa kutamani kumuona Yesu, tukimuona Yesu tutapata faraja ya kweli katika magumu yetu yote”. Kwamba, Filipo aliposikia wanataka kumuona Yesu, alijitoa na kuwakutanisha na Yesu. Je! Sisi ni mara ngapi tunafanya hivyo? Aidha, alifafanua kwa kusema kuwa “ Familia hii ya Shaidi ninayoifahamu kwa kiasi, wa hapa Chome na hata wa Vudee! Nimeona wakifanya juhudi za kuwapeleka watu kwa Yesu. Wanahubiri neno la mungu na pia wanatumia mali zao kuwafikisha watu kwa Yesu”. Alimalizia kwa kusema “Yesu ndio faraja ya kweli na huwafungulia vifungo vyenu ni budi kumfuata yeye”. Aidha familia ilikuwa imechagua wimbo Na. 283 unaosema Bwana Yesu yuko wapi kwa kusindikiza sadaka katika ibada.

Aidha, katika kutoa salamu kwa familia baba Askofu alieleza kuwa, ukipitia kumbukumbu za kuanzishwa kwa Uaskofu na hirakiya yake utaona kuwa ulianzishwa na mzee Abrahamu Shaidi. Aliacha swali la kujiuliza kwa wanafamilia “je! Sisi tumefanya nini?”. Na katika salamu hizo alihitimisha kwa kuomba kuwa wainuliwe akina Abrahamu wengi katika ukoo.

Kumaliza msiba: Wazee .Nkombole na …Nkombolwe waliratibisha zoezi la kumaliza msiba na kuwaruhusu akina mama wakiongozwa na ……. Kukamilisha shughuli ya kugawa nguo na vitu vya marehemu mama/bibi yetu. Kazi hii ilikuwa na huzuni na vilio hasa pale watoto na wajukuu walipokuwa wakigawiwa nguo. Nyimbo mbalimbali alizokuwa anapenda bibi ziliimbwa wakati zoezi hili lilipofanyika na kukamilika katika upendo mkubwa.

Kikao kifanyika siku hiyo hiyo baada ya chkula cha mchana jumamosi jioni na kufanya tathmini ya shughuli nzima iliyofanyika b