• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
service photo

KUMALIZA MSIBA WA MAREHEMU YONAZI SHAIDI NZIAMWE KISIWANI 12/09/2020

IBADA: Ibada itaongozwa na viongozi wa kanisa ,Ibada hiyo itafuatiwa na kusimikwa kiongozi wa familia.

KUSIMIKA KIONGOZI WA FAMILIA

Tuanze tendo hili la kumsimika kiongozi wa familia ya marehemu baba yetu Yonazi Shaidi Nziamwe kwa kuimba wimbo

Wakati tunaimba wimbo huo familia ya marehemu (Yonazi Shahidi) ipite mbele.

PENDEKEZO LA KIONGOZI: Jina la mwanafamilia anayependezwa kuwa kiongozi wa familia hii litajwe.

ITIKIO: Wanafamilia hii waulizwe kama wanakubaliana na pendekezo hilo,ikiwa itikio ni ndiyo mhusika anaweza kusimikwa baada ya yeye mwenyewe kukubali.

KIONGOZI: Je, unakubali kupokea wajibu huu wa kuwa kiongozi wa familia hii?

MILA NA DESTURI: Kulingana na mila na desturi za Kipare ungepewa vifaa vya kimila alivyokuwa akitumia marehemu kama vile kofia, fimbo, upinde na mishale ikiwa ndani ya poda lake. Kofia,koti na fimbo ni alama ya kuonyesha kuwa umepewa mamlaka ya kuongoza familia hiyo,Upinde na mishale ni alama ya kuonyesha kuwa wewe ndio mlinzi na mwangalizi wa familia hiyo na kwamba utasimamia usalama na ustawi wa familia hiyo. Badala ya kutumia utaratibu huu wa mila na desturi hizi za kipare tumeamua kukusimika kulingana na Neno la Mungu.Neno la Mungu linapumzi yake na tena lafaa kwa mafundisho.

MAMLAKA : Tunakupa mamlaka ya kuongoza familia hii kwa neno la Mungu kutoka Marko 10:42-45, 1 Timotheo 5:1-2, iWakorintho 3:18-20, Yakobo 3:17,Mathayo 5:14-16, 1Petro 2:17,kutoka 18:21 Wafilipi 2:3-5,Hesabu 27:15-17,Luka 22:26-27,Tito 2:6-8 1Timotheo 5:17 (walioandaliwa wasome vifungu hivyo vya Biblia)

ULINZI: Tunakuombea ulinzi wa familia hii kwa Neno la Mungu kutoka kumbukumbu la Torati 31:6,Yoshua 1:9,10:25 1Wakorintho 16:13, Zaburi 31:24, 2Timotheo 1:7,Waefeso 6:10,2Wakorintho 10:3-5 1Petro 4:1-1(walioandaliwa wasome vifungu hivyo vya Biblia).

UPENDO: Tunakuombea kwa Mungu usimamie familia hii kwa upendo na kwa haki bila ya upendeleo wowote,Tunakupa Neno la Mungu litakalokuongoza kutokaWarumi 12:9-10,Yohana 13:34-35, 15:9-14,1Wakorintho 13:1-8 Wagalatia 5:13-15, Wakolosai 3:14-17, 1Timotheo 5:8,2Timotheo 2:24-26, 1Petro 4:8-11 Zaburi 11:7,17:1-2,Mithali, Warumi 1:17-18, 1Waebranic 10:38-39,Wagalatia 2:16 (walioandaliwa wasome vifungu hiyo)

KIONGOZI: Kiongozi amkabidhi bahasha yenye maneno yote ya Mungu aliyosomewa.

MAOMBI: Maombi yaongozwe na Mchungaji/Mwinjilisti au mtumishi au Mzee wa kanisa

MWISHO : SHUKRANI YA FAMILIA