• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
service photo

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU ANAELI AMINI SHAIDI

• KUZALIWA

Marehemu Anaeli Amini Shaidi alizaliwa tarehe 28/02/1946 huko Vudee Mpinji akiwa ni mtoto wa 2 kati ya watoto 10 wa Mzee Nakaza Nzota na Bibi Manaeli Kisimbo

• UBATIZO

Marehemu Anaeli Amini Shaidi alibatizwa tarehe 31/3/1946 kwenye kanisa la K.K.K.T Usharika wa Vudee.

• ELIMU

Marehemu Anaeli Amini Shaidi alipata elimu yake kwenye shule ya msingi Vudee kuanzia mwaka 1953-1956.Mwaka 1963 alijiunga na chuo cha maarifa ya jamii Manka hadi 1965 alipohitimu katika fani ya U-Parish Worker na upishi.

• NDOA

Marehemu Anaeli Amini Shaidi alifunga ndoa takatifu na Amini Ghuheni Shaidi mnamo tarehe 25/10/1965 katika kanisa la K.K.K.T usharika wa Vudee na kujaliwa kupata watoto 6 wakiume 2 na wa kike 4.Marehemu Anaeli Shaidi ameacha wajukuu 13 na vitukuu 6. Wakati wa uhai wake, marehemu Anaeli Amini Shaidi licha ya kuwa mama na mlezi wa familia pia alijishughulisha na;

• Kilimo

• Kufundisha shule ya watoto ya Jumapili kwa miaka 8

• Kuimba kwaya ya usharika ya Vudee

• UGONJWA

Marehemu Anaeli Amini Shaidi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Athsma (pumu) kwa zaidi ya miaka 50 ambayo alitibiwa kwenye hospital za wilaya, mkoa na rufaa zikiwemo za Same, Seliani na Muhimbili kwa nyakati tofauti.

Hali ya marehemu ilianza kubadilika kuanzia mwezi Machi 2021 ambapo alilazwa kwenye hospital za Meru, Same na KCM. Alifariki tarehe 29/5/2021 katika hospital ya KCMC- Moshi.

SHUKRANI

• Tunawashukuru watumishi wa Mungu kutoka madhehebu mbalimbali ambao walikuwa wakimuombea na kumtia moyo wakati wote.

• Tunawashukuru madaktari,manesi na wauguzi wa hospital zote alizotibiwa.

• Tunawashukuru ndugu wote, jamaa na marafiki na majirani walioshiriki kwa hali na mali katika kipindi chote cha ugonjwa wake.

• Shukrani za pekee ziende kwa ndugu yetu Jemsi Stankey Mchome ambaye alikuwa ni mtoto na rafiki mwaminifu kwa marehemu mama yetu Anaeli Shaidi kwa miaka yote, Mungu ambariki

BWANA AMETOA,BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE AMEN.