SADAKA YA SHUKRANI YA UKOO – CHOME 29/09/2019
Utangulizi
Ukoo wa Shaidi unapatano la kumtolea Mungu sadaka ya shukrani kila baada ya miaka miwili. Sadaka hii inatolewa katika madhabahu ya BWANA katika kijiji cha Vudee au Chome. Tarehe 29/09/2019 wana ukoo walisimama mbele ya madhabahu ya BWANA katika usharika wa Chome na kumtolea BWANA sadaka zao.
Maandalizi.
Maandalizi ya siku hii ya kutoa sadaka yalifanyika katika vikao mbalimbali vilivyoongozwa na Mwenyekiti Huruma A. Shaidi, Katibu Samson E. Shaidi na Mtunza fedha Anna Ngoo .Viongozi hawa waliratibu vizuri maandalizi yote na walisimamia shughuli zote zilizohusu utoaji wa sadaka ya ukoo. Ziliundwa kamati za maombi, usafiri na chakula .Kamati hizi zote zilifanya kazi zake kwa bidii na kwa uaminifu.
Matoleo
Ukoo ulikubaliana kuwa kuwe na aina mbili za sadaka moja kwa ajili ya wahitaji na nyingine kwa ajili ya huduma za kanisa. Sadaka ya wahitaji itolewe katika ibada itakayofanyika nyumbani Chome tarehe 28/09/2019 na sadaka kwa ajili ya huduma za kanisa itolewe kanisani Chome tarehe 29/09/2019. Matoleo mengine yalitolewa kama michango kwa ajili ya matumizi ya usafiri pamoja na chakula. Kikao kilikubaliana kuwa matoleo kwa ajili ya sadaka yasiwekewe kiwango bali kila mtu atoe kwa jinsi ambavyo Mungu amembariki yeye na familia yake. Michango kwa ajili ya matumizi ilipangwa kuwa kiwango cha chini kiwe ni shs 200,000/= (laki mbili) kwa wajukuu wa Shaidi na kiwango cha chini kwa vitukuu wa Shaidi kiwe shs 50,000/=. Jumla ya shs 11, 985,000/= zilipatikana.
Ibada Chome 28/09/2019
Tunamshukuru Mungu kwa kuwa safari ya wanaukoo wote kwenda Chome aliiratibu Mungu mwenyewe. Watu wote walifika Chome salama wakimsifu na kumshukuru Mungu.Ibada iliyofanyika nyumbani iliongozwa na Mch.Kiongozi wa K.K.K.T –Usharika wa Chome, Mch. Mbazieli Y. Kirumbi akisaidiwa na Mchungaji Wilson Makame(mstaafu).
Katika ibada hii wanaukoo na waalikwa wote walimsifu Mungu kwa nyimbo wakiongozwa na kwaya ya Uinjilisti Chome .Mch.Kirumbi alifundisha Neno la Mungu kutoka Luka 15:11-32 akisisitiza upendo na umoja katika Kristo Yesu, Bwana wetu. Ibada hii iliambatana na kutoa sadaka kwa wahitaji. Kanisa lilishirikishwa katika kuwapata wahitaji kwelikweli; wajane, yatima, na wenye mahitaji maalum. Wahitaji wote walialikwa ndani na baada ya Mchungaji kuombea sadaka hizo alimgawia kila mmoja kulingana na utaratibu uliowekwa jumla ya shs 3,400,000/= (milioni tatu laki nne) zilitolewa kwa wahitaji. Tunamshukuru Mungu na tunamrudishia sifa, heshima na utukufu kwa tendo hili kubwa alilotutendea. Baada ya ibada wanaukoo na waalikwa wote walishiriki chakula cha mchana.
Ibada Chome 29/09/2019
Tarehe 29/09/2019 siku ya Jumapili wanaukoo waliofika Chome waliingia ibada ya kwanza iliyoanza saa mbili asubuhi hadi saa 4 asubuhi katika kanisa la KKKT-Usharika wa Chome. Ibada iliongozwa na Mch. Kirumbi akishirikiana na Mwinjilisti Julijesita Richard. Neno la Mungu lilifundishwa na mtumishi Nakazaeli Elirehema Mndeme. Iikuwa ibada njema ya kumsifu na kumwabudu Mungu. Katika ibada hii wanaukoo walimtolea BWANA sadaka ya ukoo na sadaka zao zingine wakiongozwa na Wilfred A. Shaidi. Jumla ya shs 5,150,000/= zilitolewa kanisani kwa ajili ya kazi ya Mungu. Katika ibada hii wanaukoo walipata nafasi ya kipekee kabisa ya kuchangia kwaya ya Uinjilisti kwa ajili ya kurekodi nyimbo za kumsifu Mungu. Tendo hili liliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Sirieli E. Shaidi (Mrs. Dr. Mchembe). Kwaya ilikuwa na mahitaji ya shs 2,000,000/= (Milioni mbili lakini wanaukoo waliweza kuwachangia shs…………………. kati ya hizo tasilimu zilikuwa shs………………. na ahadi shs………………………Tunamshukuru Mungu kwa kutupa nafasi ya kumtumikia kwa njia hii.Baada ya ibadaa wanaukoo pamoja na waalikwa wote walifika nyumbani na kupata kifungua kinywa na kisha wanaukoo walianza safari ya kurudi makwao. Tunamshukuru Mungu kwa kuwa Mungu wetu ni mwaminifu aliyesafiri pamoja nao. Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi Israeli naaseme sasa. Shukrani inayofuata itolewe mwaka 2021 katika usharika wa Vudee. Tunamwomba Mungu atubariki ili wakati huo ukifika tusimame mbele ya madhabahu yake na kumtolea sadaka zitakazompendeza.