• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
  • 23 Aug, 2023
  • Admin

 PRAYER ITEMS
Wapendwa katika BWANA nawasalimu katika jina lipitalo majina yote, jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. 
Shukrani tutakazotoa wakati wa Pasaka zitaambatana na maombi yetu kwa Mungu. Tumuombe Mungu mambo makuu yafuatayo. 
1.Tuombe tukae nyumbani mwa BWANA milele. Tukae kwa umoja, amani, upendo na furaha (Zab. 23:6).
2.Tuombe hekima, maarifa, akili na ujuzi (Kutoka 31:3).
Katika Prayer items hizi tutaendelea kujifunza vipengele mbalimbali vya kusimamia maombi yetu.

1.1UMOJA 
Katika umoja kuna baraka za Mungu. (Zab. 133:1,3). Tazama jinsi ilivyo vema na kupendeza ndugu wakae pamoja, maana ndiko BWANA alikoamuru baraka, Na uzima wa milele. 

1.2AMANI.
Tuombe amani ya Mungu ipitayo akili zote katika Kristo Yesu na tutafute kuwa na amani na watu wote (Wafilipi 4:7, Waebrania 12:14).

1.3UPENDO
Tumuombe Mungu upendo wa ndugu udumu siku zote za maisha yetu (Waebrania 13:1 na 13:16), kwa kuwa hii ni amri mpya kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo (Yohana 13:34) Tukipendana sisi kwa sisi watu wote watatambua ya kuwa sisi ni wanafunzi wa Bwana wetu Yesu Kristo (Yohana 2:8 – 11).

1.4    FURAHA
           Tuombe tuwe na furaha siku zote katika Bwana wetu Yesu Kristo (Wafilipi 4:4 – 6). Ndipo vinywa vyetu vitakapojaa vicheko na ndimi zetu kelele za furaha kwa kuwa BWANA ametutendea mambo makuu.
Nawakaribisha tuendelee kutafakari prayer items zetu. Nitaendelea kutafakari prayer items namba 2 pamoja nanyi.

Ndugu zangu, Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo ikae nasi sote tunapotafakari kuhusu kumtolea Mungu shukrani zetu za Pasaka pamoja na maombi yetu kwa Mungu. Leo tutatafakari Prayer Item yetu Namba 2.

1.0 PRAYER ITEM 2
  Tumwombe Mungu sisi na uzao wetu atupe hekima maarifa,akili na ujuzi( Kutoka 31:3). Mungu atujaze Roho wake, katika hekima, na maarifa na ujuzi na mambo ya kazi ya kila aina (Kutoka 35:31)

1.1 HEKIMA
     Tumwombe Mungu atupe hekima, itokayo kwake Yakobo 3:17 “Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi,tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, Imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki”. Tumwombe Mungu wana wa uzao wetu wakue, waongezeke nguvu,wajae hekima, na neema ya Mungu iwe juu yao ( Luka 2:40).

1.2 MAARIFA
      Tumwombe Mungu atujaze sisi na uzao wetu maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni na kuzidi katika maarifa ya Mungu ( Wakolosai 1:9 -10). Tusije tukaangamia kwa kukosa maarifa au kwa kukataa maarifa kutoka kwa Mungu wetu ( Hosea 4:6). Kwa kuwa tukifanya hivyo Mungu atatukataa tusiwe makuhani wake.

1.3 AKILI
      Tumwombe Mungu atupe akili katika mambo yote, na atupe akili ya kuyafahamu maandiko, yaani Neno lake (2 Timotheo 2:7) “Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.” Luka 24:46 “Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.” Akili Mungu atakazotupa zitusaidie kuomba kwa akili na kuimba kwa akili. (Wakorintho 14:15) “Imekuwaje basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia. “Akili tunazoziomba kwa Mungu zimsaidie kila mmoja wetu kumpenda Bwana Mungu wetu kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kwa akili zake zote, na kwa nguvu zake zote ( Marko 12:30).

1.4 UJUZI
     Tumwombe Mungu atupe ujuzi unaopatikana katika Neno lake, atuzidishie neema yake katika hekima yote na ujuzi (Waefeso 1:8) Ujuzi Mungu atakaotupa utusaidie tuzae matunda kwa kila kazi njema. 

Share This