• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
  • 22 Aug, 2023
  • Admin

Maombi na Maombezi kwa ajili ya kiongozi anayesimikwa

 

Neno la Mungu linatutaka kufanya maombi na maombezi kwa ajili ya watu wengine, viongozi wa jamii, wasiookolewa, wakristo wenzetu kanisa na wahudumu wake. Katika jambo hili maombi na maombezi yafanyike kulingana na jinsi roho wa Mungu atakavyowaongoza viongozi wa ibada.

1Timotheo 2:1. Basi kabla  ya mambo yote nataka dua, na sala, na maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote, kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka , tuishi maisha ya utulivu na amani katika utauwa wote na ustahivu .Hili ni zuri nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu , ambaye hutaka watu wote waokolewe na kupata kujua yaliyo kweli.

Waefeso 6:17-18. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu,na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu ;kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho ,mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.

Mwanzo 24:12.Naye akasema,Ee Bwana,Mungu wa bwana wangu Ibrahimu nakuomba mambo yangu uyajalie yawe heri leo,ukamfadhili bwana wangu Ibrahimu.

Mwanzo 25:21. Isaka akamuomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa.Naye BWANA akamwitikia na Rebeka mkewe akachukua mimba.

1Samweli 12:23-25. Walakini mimi, hasha nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi, lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema na kunyoka .Mcheni BWAN tu mkamtumikie kwa kweli kwa mioyo yenu yote, maana kumbukeni jinsi alivyowatendea mambo makuu.Lakini kama mkiendelea kutenda  mabaya ,mtaangamia , ninyi na mfalme wenu pia

Mathayo 19:13-15. Ndipo akaletewa watoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombea, wanafunzi wake wakawakemea. Lakini Yesu akasema, waacheni watoto wadogo waje kwangu wala msiwazuie, kwa maana walio mfano wa hao ufalme wa mbinguni ni wao .Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko.

Luka 1:13. Lakini yule malaika akamwambia usiogope Zakaria maana dua yako imesikika na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume na jina lake utamwita Yohana.

  

Luka 22:31-32. Akasema Simon, Simon tazama Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike, nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.

Luka 23:34.Yesu Kristo anatufundisha kuwaombea watu wengine kama alivyofanya pale msalabani aliposema Baba uwasamehe kwa kuwa hawajui watendalo.

Yohana 14:13-17. Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu hilo nitalifanya ili Baba atukuzwe ndani ya mwana .Mkiomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya, Mkinipenda mtazishika amri zangu .Nami nitamwomba Baba,  naye atawapa Msaidizi mwingine ili akae nanyi hata milele;  ndiye Roho wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea kwa kuwa haumwoni wala haumtambui bali ninyi mnamtambua ,maana anakaa kwenu naye atakuwa ndani yenu.

Yohana 17:9-10, 15-21. Mimi nawaombea hao,siuombei ulimwengu bali hao ulionipa kwa kuwa hao ni wako na wote walio wangu ni wako na walio wako ni wangu nami nimetukuzwa ndani yao. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu uwatakase kwa ile kweli, neno  lako ndilo kweli. Wala sio hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe Baba ulivyo ndani yangu , nami  ndani yako nao wawe ndani yetu , ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

Matendo ya Mitume 12:5

Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. Hata Petro alipopata fahamu akasema, sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi.

Matendo ya Mitume 14:23. Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa na kuomba pamoja na kufunga wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.

Warumi 8:26-27. Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo ,lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

Warumi 10:1-2. Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu na dua yangu nimwombayo Mungu ni kwa ajili yao ili waokolewe. Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.     

Warumi 15:30-33. Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu, kwamba niokolewe na wale wasioamini katika Uyahudi, na tena huduma yangu niliyo nayo huko Yerusalem, ikubalike kwa watakatifu, nipate kufika kwenu kwa furaha,  kama apendavyo Mungu , nikapate kupumzika pamoja nanyi. Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amina.

Wakolosai 4:2-4. Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani , mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa ili niidhihirishe kama inipasavyo kunena.

1Wathesalonike 5:25-27. Ndugu, tuombeeni wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu. Nawaapisha kwa Bwana, ndugu wote wasomewe waraka huu .Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.

2Wathesalonike 1:1-2, 11-12. Paulo na Silwano na Timotheo kwa Kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba yetu na Bwana Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo. Kwa hiyo twawaombea ninyi siku zote, ili Mungu wetu awahesabu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu; Jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na  ya Bwana Yesu Kristo.

Wathesalonike 3:1-2, Hatimaye ndugu tuombeeni neno la Bwana liendelee na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya, maana si wote walio na imani.

Tuhitimishe sehemu hii ya kuwaombea viongozi wanaosimikwa kwa kuwaasa kwa maneno haya. Jifunze nafsi yako na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia. Tuseme kwa pamoja maneno haya;

Mbarikiwa ni wewe Bwana Mungu wetu uliyeziumba mbingu na nchi, Mungu wa milele, unayeishi katika vizazi vyote. Wewe ni asili ya hekima takatifu na chemchemi ya ukweli. Tunakushukuru kwa ajili ya viongozi wa aina mbalimbali miongoni mwetu wenye mfano wa kuigwa kwa maisha na utendaji wao. Tuwezeshe kufuata mfano wao tunapokutumikia kwa utayari na umoja wa moyo. Kwa Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wetu.Ameni.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                          

Share This