WIMBO ULIO BORA 1:1-6, 2:1-2, 2:16-17, 3:1-4, 4:1-2, 7,5:6,9-11 na 8:1
Wimbo ulio bora wa Suleimani. Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pambaja zake zapita divai, manukato yako yanukia vizuri, Jina lake ni kama marhamu iliyomiminwa,wanawali hukupenda kwa hiyoameniingiza mfalme vyumbani mwake .Tutafurahi na kukushangilia, tutazinena pambaja zako kuliko divai.Mimi ni ua la uwandani, ni nyinyoro ya mabondeni kama nyinyoro kati ya miiba, kadhalika mpenzi wangu kati ya binti mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake; hulisha kundi lake penye nyinyoro.Hatajua lipunge, na vivuli vikimbie unigeukie, mpendwa wangu, nawe uwe kama paa au ayala, juu ya milima ya Betheri.
Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, nalimtafuta, nisimpate .Nikasema, haya niondoke nizunguke mjini na viwanjani, nitamtafuta mpendwa wa nafsi yangu nikamtafuta, nisimpate.Walinzi wazungukao mjini waliniona; je, mmemwona mpendwa wa nafsi yangu.Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, nikamwona mpendwa wa nafsi yangu nikamshika, nisimwache tena, hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, chumbani aliyenizaa.Tazama u mzuri mpenzi wangu, u mzuri macho yako ni kama ya hua, nyuma ya barakoa yako.Nywele zako ni kama kundi la mbuzi, wakijilaza mbavuni pa mlima Geleadi, mpenzi wangu u mzuri pia, wala ndani yako hamna ila nalimfungulia mpendwa wangu lakini mpendwa wangu amegeuka amepita. Nimezimia nafsi yangu aliponena nikamtafuta nisimpate, nikamwita, asiniitike.Mpendwa wa namna gani ni mpendwa wako, wewe uliye mzuri katika wanawake.Mpendwa wa namna gani ni mpendwa wako, hata wewe utusihi hivyo mpendwa wangu ni mweupe, tena mwekundu, mashuhuri miongoni mwa elfu.Kichwa chake ni kama dhahabu safi sana, nywele zake ni za ukoka, nyeusi kama kunguru laitiungekuwa kama ndugu yangu, aliyenyonya matiti ya mamangu, kama ningekukuta huko nje, ningekubusu, asinidharau mtu
Utangulizi
Wimbo Ulio Bora ni kati ya vitabu vya Biblia vya kishairina cha kipekee zaidi kwa kuwa kinaimba mahaba ya wapenzi wawili mume na mke au bwana na bibi harusi.Pamoja na kusifiana uzuri wa maumbo ya nje yaani maumbile yao , tunaona upendo mkubwa kati yao .Ni jambo jema mume au mke kumsifu mwenza wake lakini zaidi ya yote wapendana na wamsifu kwa pamoja Bwana harusi wetu, Yesu Kristo na tena wampende .Neno la Mungu linawaagiza waume kuwa wawapende wake zao .Waefeso 5:28-29 “ Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe.Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe .Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote ; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake”.Katika tafakari ya mistari iliyonukuliwa hapo juu tutaufananisha upendo wa wapenzi hawa na upendo kati ya Yesu Kristo na Kanisa lake. Waefeso 5:22-26 “Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu , kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa, naye ni mwokozi wa mwili .Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.Enyi waume wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa , akajitoa kwa ajili yake ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa ajili yake ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno.Neno la Mungu linatufundisha kuwa ndiye kichwa, yaani cha Kanisa naye ni mwanzo ni mzaliwa wa kwanza katikawafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote .Ufunuo 21:9-10 “ Akaja mmoja wa wale Malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami akisema , Njoo huku nami nitakuonyesha yule Bibi harusi mke wa mwana Kondoo .Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu. Pamoja na mafundisho mengi yanayoweza kupatikana katika mistari hii leo tutaangalia mambo makuu matatu kuhusu wapenzi hawa :-
1. Watafurahi na kushangilia na ndani mwao hakutakuwa na ila
2. Watashiba na kuburudika,
3. Watafuatana , watashikana nahawataachana tena hata kama watapigwa na kutiwa jeraha
Mambo yote haya matatu yanapatikana ukiwa ndani ya Kristo Yesu.
Tutafurahi na kushangilia katika YESU KRISTO ambaye ndani yake hakuna ila.
Tunatakiwa kufurahi na kumshangilia Bwana wetu Yesu Kristo kama jinsi ambavyo na yeye alimshangilia Baba yake;Mathayo 10:21 “Saa ile ilealishangilia kwa Roho mtakatifu, akasema.Nashukuru , Baba , Bwana wa Mbingu na nchi kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga, Naam, Baba kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza. “Nabii Isaya naye alitabiri akasema, Isaya 51:11 “Nao waliokombolewa na BWANA watarejea, watafika Sayuni, wakiimba, furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao. Watapata shangwe na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia”. Tukiwa ndani ya Kristo tunatakiwa kuwa na furaha. Wafilipi 4:4-6 “Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema, furahini. Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa neno lolote bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu . Na amani ya Mungu ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu’’ 1 Wathesalonike 5:16-18 “Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu”. Pamoja na kuwa na furaha tunatakiwa tumshangilie Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo kwa kuwa ametupatia wokovu bure .1 Samweli 2:1 “Naye Hana akaomba akasema moyo wangu wamshangilia BWANA pembe yangu imetukuka katika BWANA, kinywa changukimepanuka juu ya adui zangu.Kwa kuwa naufurahia wokovu wako.Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA, kwa maana hakuna yeyote ila wewe, wala hakuna mwamba kama Mungu wetu”. Mariam naye alisema, moyo wangu wamwadhimisha Bwana, na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu (Luka 1:46-47) .Daudi alipouona utukufu wa BWANA na wokovu wake alifurahi na kushangilia kwa nyimbo za sifa na mashairi , Zaburi 20:5 “Na tuushangilie wokovu wako, kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu.Bwana akutimizie matakwa yako yote. Ili nizisimulie sifa zake zote, katika malango ya binti Sayuni, nitafurahia wokovu wako. Daudi anaendelea kuimba kuwa mataifa na washangilie, naam, waimbe kwa furaha, maana kwa haki utawahukumu watu na kuwaongoza mataifa walioko duniani.Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha. Zaburi 96:11-13 “Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie, bahari na ivume na vyote viijazavyo. Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo, ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha .Mbele za BWANA, kwa maana anakuja, kwa maana anakuja aihukumu nchi.Atahukumu ulimwengu kwa haki na mataifa kwa uaminifu wake” Mungu wetu ni mwenye haki asiye na ila na sisi ambao tupo ndani yake hatutakuwa na ila.Yesu Kristo alijitoa kwa ajili ya Kanisa ili makusudi alitakase na kulisafisha kwamaji katika neno (Waefeso5:26-27) apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.Wafilipi 2:15 “Mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati yao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu “Tukishika neno lake la uzima tutaona fahari katika siku ya Kristo.Ufunuo 19:7-9 “Na tufurahi, tukashangilie, tumpe utukufu wake; Kwa kuwa harusi ya mwana kondoo imekuja na mkewe amejiweka tayari.Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo safi, kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. “Katika furaha na mashangilio haya tutashiba na kuburudika ndani ya Yesu Kristo, Bwana wetu.
Tutashiba na kuburudika ndani ya Yesu Kristo , Bwana wetu kwa kula na kunywa maji ya uzima
Mungu hapo mwanzo alivyomuumba mwanadamu alimuandalia chakula cha kutosha kula na kushiba na maji ya kunywa Mwanzo 1:29 Mungu akasema , tazama nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti ambao matunda yake yana mbegu, vitakuwa ndivyo chakula chenu. Tunaona pia katika nyakati mbalimbali Mungu aliwalisha wana wa Israel jangwani, aliwalisha manabii wake, mitume na watakatifu wake kwa kutumia njia mbalimbali. Bwana Yesu aliwalisha makutano elfu tano kwa mikate 5 na samaki 2 wakashiba na kubakisha vikapu kumi na viwili.Mungu Baba mwenye enzi yote ashukuriwe kwa kutupatia mkate wetu wa kila siku hata leo hii. Katika somo hili tutajikita zaidi kuona jinsi Mungu anavyotupatia chakula cha kiroho kiletacho wokovu na maji yaletayo uzima wa milele.
Yohana 6:26-29, 40-56, “Yesu akawajibu, akasema,Amin, Amin nawaambieni; Ninyi mnanitafuta, si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba. Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu. Basi wakamwambia, tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia; hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye.Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya , kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.” Basi Wayahudi wakamunung’unikia kwa sababu alisema, mimi ni chakula kilichoshuka kutoka mbinguni. Wakasema, Je, huyu siye Yesu, mwana wa Yusufu ambaye twamjua babaye na mamaye? Sasa asemaje huyu nimeshuka kutoka mbinguni? Basi Yesu akajibu akawaambia, msinung’unika ninyi kwa ninyi. Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyempleleka, nami nitamfufua siku ya mwisho. Amin, amin, nawaambia Yeye aaminiye yuna uzima wa milele. Mimi ndimi chakula cha uzima.Baba zenu waliila mana jangwani, wakafa. Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife. Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule? Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, msipokula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.’’ Tukikaa ndani ya Yesu tukimwamini na kushika neno lake tutashiba na tutaburudika kwa kunywa maji ya uzima. Yesu alipokutana na mwanamke Msamaria kisimani alimwomba ampe maji anywe,yule mwanamke aliposita Yesu akamwambia, kama ungalijua anayekuomba maji ni nani ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai.Yesu akamwambia kila anwaye maji haya ataona kiu tena; walakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchem ya maji ya kibubujikia uzima wa milele (Yohana4:7-14). Yesu anatukaribisha anasema mtu akiona kiu, na aje kwake anywe.Yohana 7:37-41 “Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye, kwa maana roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa” Heri wenye njaa na kiu ya haki maana hao watashibishwa. Hawa ni wale wenye njaa n akiu ya neno la Mungu aliye hai. Maji ya uzima ambayo ni neno la Mungu yanapatikana bure kwa wote waamini kuwa Mwana yuna uzima wa milele na asiyemwamini mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia. Tumwombe Roho Mtakatifu wa Mungu atufundishe mapenzi ya Mungu na atuongoze katika kweli yote, tujue jinsi ya kumfuata Bwana wetu Yesu Kristo na kushikamana naye siku zote za maisha yetu.
Tutamfuata Bwana wetu Yesu Kristo na kushikamana naye na tusimwache hata wakati wa mateso.
Yesu Kristo anataka tuache vitu vyote na kumfuata yeye kwanza na vingine vyote tutaongezewa.Alipowaita wanafunzi wake wa kwanza hakuwataka kuondoka na kitu chochote bali aliwaambia, Nifuate nao wakaondoka wakamfuata.Yesu alimwambia Petro nifuate nami nitakufanya kuwa mvuvi wa watu. Petro alimfuata Yesu na kuacha vitu vingine vyote, na hakika maisha yake yakawavuta watu wengi kwa Kristo. Luka Mtakatifu 18:28-30 “Petro akasema, (mbele ya Bwana Yesu) tazama, sisi, tumeviacha vitu vyetu vyote na kukufuata. Akawaambia hakika nawaambia, hakuna mtu aliyeacha nyumba au mke au ndugu au wazazi au wana kwa ajili ya ufalme wa Mbinguni asiyepokea zaidi mara nyingi katika zamani hizi, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.” Bwana Yesu anaendelea kuwafundisha wanafunzi wake pamoja na sisi sote leo hii katika Luka 9:23-26 “Akawaambia wote mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate .Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza au kujipoteza mwenyewe. Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo atakapokuja katika utukufu wake na wa baba na wa malaika watakatifu “Mtu yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma ya Yesu Kristo, hawezi kuwa mwanafunzi wake. Tukumbuke kuwa Bwana wetu Yesu Kristo aliubeba msalaba wake, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam mauti ya msalaba kwa ajili ya dhambi zetu. Kwa maana hii ndiyo damu yake ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. Yesu Kristo ni dhabihu kamili na ya mwisho kwa ajili ya dhambi zetu, ili afanye upatanisho kati yetu na Mungu kwa kulipa adhabu ya dhambi za wote ambao wanamwamini kwamba ni Bwana na Mwokozi wa maisha yao.
Katika kumfuata Bwana Yesu tunaweza kupata maudhi, mateso kuwekwa gerezani na hata kuuawa kwa ajili yake.Je sisi nasi tutazitoa nafsi zetu kwa ajili yake? Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. Wafilipi 1:29 “Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake, “Mtume Paulo katika Wakolosai 1;24 anasema “Sasa nafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu, tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani kanisa lake’’, Neno la Mungu linaeleza wazi wazi ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi (Matendo ya Mitume 14:22). Wakawakamata Paulo na Sila wakawavua nguo zao kwa nguvu wakatoa amri wapigwe kwa bakora na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi wakawatupa gerezani wakaamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. Biblia inayo mifano mingi ya watu waliopata mateso kwa ajili ya kumfuata Yesu Kristo. Swali la kujiuliza ni kuwa tutawezaje kushinda majaribu haya? Warumi 8; 11 “Lakini ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa roho wake anayekaa ndani yenu” Mateso ya mwenye haki ni mengi lakini BWANA humponya nayo yote roho wa Mungu anatusaidia na na anatupa nguvu tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twastahimili, tukisingiziwa twasihi kwa upendo. Tukikaa katika neno la Mungu tutakuwa wanafunzi wa Yesu kweli kweli na tena tutaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itatuweka huru. Heri astahimiliye majaribu, kwa sababu akiisha kukubaliwaataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. Tushikamane na Yesu Kristo Bwana wetu kwa kuwa hatuna mahali pengine pa kwenda penye maneno ya uzima. Kwa kuwa Mungu alimkirimia jina lile lipitalo kila jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.