• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
  • 24 Nov, 2024
  • Admin

SADAKA YA MZALIWA WA KWANZA

Bwana wetu Yesu Kristo asifiwe. Malimbuko ni sadaka inayotolewa kwenye kitu cha kwanza kupatikana au kuzaliwa au zao la kwanza.

Yesu Kristo ndio mzaliwa wetu wa kwanza na ndio sadaka wetu aliyetolewa na Mungu ili atuokoe kutoka dhambini. Wakolosai 1:15 “ Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana’’Yesu  Kristo ni limbuko lao waliolala. I Wakorintho 15:20 “ Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala’’ Kama sio Mungu kumtoa awe sadaka ya kwanza (limbuko) sisi wengine tusingepata hiyo baraka ya kufufuliwa na kuishi naye milele. Kwa hiyo tunalo tumaini la ufufuo kwa sababu yeye amefanyika kuwa sadaka wetu. Yesu Kristo ameshafanyika pasaka wetu kwa damu yake iliyomwangika pale msalabani Calvary. Hatuna haya tena ya damu ya mafahali na mbuzi kwa kuwa haiwezi kuondoa dhambi. Yesu Kristo ndiye mzaliwa wetu wa kwanza kwa watu wote, maana katika Yeye utimilifu wote wakaa. Wakolosai 1:18 “ Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani cha kanisa, naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae.’’

Tunamshukuru Mungu kwa upendo wake mkuu,upendo wa Agape kwa kumtoa Mwanawe mpendwa na wa pekee Yesu Kristo akatufia pale msalabani ili kila mtu amwaminiye asipotee,bali awe na uzima wa milele.

Katika sehemu inayofuata tutatafari kuhusu sadaka ya mzaliwa wa kwanza kwa wanadamu na wanyama.

Share This