NITAYASIMULIA MATENDO YAKO YOTE YA AJABU
Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu. Je, wewe una jambo gani la kusimulia? Zab. 118:17 Daudi anasema sitakufa bali nitaishi, nami nitayasimulia matendo ya BWANA .Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako mchana kutwa maana sijui hesabu yake (Zab 40:05). Na ulimi wangu utanena haki yako na sifa zako mchana kutwa (Zab:35:28).
Tunaweza kusimulia matendo ya BWANA ya ajabu kwa njia ya kutoa ushuhuda juu ya mambo makuu na ya ajabu Mungu aliyokutendea wewe mwenyewe, familia yako na watu wengine unaowafahamu.Ushuhuda wako uwe kwa ajili ya kuimarisha watu wengine huku ukimrudishia Mungu sifa, heshima na utukufu.
Unaweza kusimulia matendo makuu ya Mungu na ya ajabu kama yanavyo patikana katika neno lake.Neno la Mungu lina matendo makuu na ya ajabu mengi sana kuanzia Agano la kale hadi Agano Jipya. Kuanzia uumbaji wa mbingu na nchi hadi ufunuo wa kurudi kwaBwana wetu Yesu Kristo. Zab.106:2 “Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya BWANA,Kuzihubiri sifa zake zote,Ee Bwana Mungu umefanya kwa wingi miujiza yako na mawazo yako kwetu, hakuna awezaye kufananishwa nawe,kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri ni mengi sana hayahesabiki.Je? mimi na wewe tumesimulia mangapi?. Katika Zaburi 71: 15-17 Mfalme Daudi anasema Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako mchana kutwa,maana sijui hesabu yake,Nitakuja na mambo ya ajabu ya BWANA Mungu.Nitawakumbusha watu haki yako wewe peke yako. Ee Mungu umenifundisha tokea ujana wangu,Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo. Matendo makuu ya BWANA yasiposimuliwa yanaweza kusahauliwa na vizazi vyetu.Tumuombe Mungu kama mfalme Daudi tukaseme, Zaburi 71:18. “Na hata nikiwa mzee mwenye mvi, Ee Mungu,usiniache”.Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, na kila atakaye kuja uweza wako.Usione aibu kusimulia na kukiri matendo makuu ya BWANA. Ukisimulia matendo makuu ya BWANA na ya ajabu inakusaidia kuimarisha Imani yako kwa Mungu.Ukipatwa na shida kumbuka mambo makuu na ya ajabu aliyoyatenda BWANA. Je? atashindwaje hilo la kwako wewe? Kumbuka hakuna neno gumu la kumshinda BWANA.Maneno haya yakutie ujasiri na yaongeze Imani yako kwa Mungu.