NITAFURAHI NA KUKUSHANGILIA WEWE. NITALIIMBIA JINA LAKO WEWE ULIYE JUU.
Tendo la kutoa sadaka ya shukrani kwa Mungu linaambatana na furaha, mashangilio, zaburi na nyimbo za kusifu na kuabudu. Tunashangilia kwa sababu BWANA ametutendea mambo makuu na ya ajabu .Tunafurahi na kumshangilia Mungu kwa kuwa ametembea nasi kwa uaminifu mkubwa katika safari yetu ya kutafuta elimu akatufanikisha kwa kiasi kikubwa. Tumeona mafanikio makubwa katika elimu.Tunafurahi na kushangilia kwa sababu Mungu ametusimamia na kutuvusha darasa hadi darasa, kidato hadi kidato, chuo hadi chuo na mwishowe ametuvisha joho la heshima na ushindi. Halikuwa jambo rahisi kama si wewe BWANA uliyekuwa pamoja nasi.
Waliotunenea mabaya kuwa hatutasoma wameaibika. Sisi tutamwimbia BWANA kama isemavyo Zab. 9:11 “Mwimbieni BWANA akaaye Sayuni,yatangazeni kati ya watu matendo yake (makuu na ya ajabu)”. Tutoe sadaka zetu za shukrani tukiimba zaburi hii “Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema kwa maana fadhili zake ni za milele .” Tulishukuru Jina lake takatifu tuzifanyie shangwe sifa zake .Tumshukuru BWANA kwa fadhili zake na maajabu yake kwa wanadamu .Tumtolee sadaka za kushukuru na kuyasimulia matendo yake kwa kuimba. Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
Nitalishukuru jina lako kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako Maana Wewe BWANA ndiwe uliye juu, Juu sana kuliko nchi yote, Umetukuka sana juu ya miungu yote (Zab 97:9).Tumwimbie BWANA wimbo mpya kwa maana ametenda mambo ya ajabu .Mshangilieni BWANA nchi yote inueni sauti imbeni kwa furaha imbeni zaburi.Shangilieni mbele ya Mfalme BWANA kwa kuwa BWANA anapendezwa na sifa na anaishi katika sifa.Pasaka 2024 Njooni tumwimbie BWANA, tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.Tuje mbele zake kwa shukrani, tumfanyie shangwe kwa zaburi. BWANA tubariki sisi sote tunaokuimbia.