MWANZO 2:8-9 “BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa, na mti wa uzima katikati ya bustani na mti wa ujuzi wa mema na mabaya”.
Katika somo hili pamoja na kuwa kuna mambo mengi ya kujifunza tutaangalia mambo makuu matatu;
Mungu alifanya kazi ya kuandaa matunda na chakula kinachofaa kuliwa kwa ajili ya Adamu na Hawa kama anavyofanya kwetu hivi leo .Hebu tuangalie BWANA , Mungu ametuandalia chakula gani kinachofaa na ambacho tunatakiwa kukila.Yohana 6:48-59. “Mimi ndimi chakula cha uzima,baba zenu waliila mana jangwani,wakafa.Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni,kwamba mtu akile wale asife.Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni,mtu akila chakula hiki, ataishi milele.Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule?
Basi Yesu akawaambia ,Amin, amin nawaambieni, msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake hamna uzima ndani yenu .Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anae uzima wa milele,nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli.Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu name ukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba.Kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni, si kama mababa walivyokula wakafa,bali akilaye chakula hicho ataishi milele.Maneno hayo aliyasema katika sinagogi, alipokuwa akifundisha huko Kapernaumu”.
Yohana 6:33-35 Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.Basi wakamwambia ,Bwana siku zote utupe chakula hiki.Yesu akawaambia ,Mimi ndimi chakula cha uzima,yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa ,naye aniaminiye hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe”.
Tunafahamu kuwa mwanadamu anahitaji aina mbili za chakula nacho ni cha kimwili na chakula cha kiroho.Chakula cha kiroho kina maana zaidi kwa kuwa kinaleta uzima wa milele. Mathayo 4:4 “Imeandikwa ,mtu hataishi kwa mkate tu,ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu”.Haya ni majibu Bwana wetu Yesu Kristo aliyoyatoa wakati akijaribiwa kule nyikani na shetani .Wakati wanafunzi wake walipomtaka ale chakula aliwajibu, “akawaambia,Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi .Basi wanafunzi wake wakasemezana,Je mtu amemletea chakula. Yesu akawambia, chakula changu ndicho hiki niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake (Yohana 4:32-34).”
Tunachotakiwa kutambua hapa ni kuwa roho ya mtu haishibishwi kwa chakula cha mwili kinachoharibika bali kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha BWANA ,Mungu wetu. Mungu ametuandalia chakula kinachofaa kuliwa nacho ni Neno ambaye ni Yesu Kristo.
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake,utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema ya kweli (Yohana 1:14).”
Katika sehemu hii ya pili tuangalie kuhusumti wa uzima katikati ya bustani ya Edeni.Neno la Mungu katika Mwanzo 3:22 “BWANA Mungu akasema ,Basi huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya na sasa asiye kunyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima akalaakaishi milele”.Mungu akamfukuza Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni na akaiwekea ulinzi mkali ili kuilinda njia ya mtu wa uzima.Katika sehemu hii tuangalie ni matunda gani tunayotakiwa kula ili tuishi milele? Na ni njia gani tuitumie kuufikia mti huo? Matunda tunayotakiwa kuyala ili kupata uzima wa milele ni kumwamini Mungu Baba,Mwana na Roho Mtakatifu na kufanya mapenzi yake .Yohana Mtakatifu 6:40 “Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho”.Tukumbuke kuwa kutenda mapenzi ya Mungu ni kushika na kutii amri na mausia yake kama yanavyopatikana katika Neno lake.Kwa maana mapenzi ya Mungu ni kuwa sisi tuwe watakatifu na tujiepushe na tamaa zote.1Yohana 2:17 Na dunia inapita pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele”.Neema ya kupata uzima wa mileleinaonyesha nikwa jinsi gani Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanae Yesu Kristokufa pale msalabani kwa ajili ya dhambi zetu kwa kuwa kwa haki yetu wenyewe hatuwezi, ili kila amwaminiye apate uzima wa milele (Yohana 3:16) .Yesu Kristo anasema kuwa kwa maana saa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini watasikia sauti yake.Nao watatoka wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu (Yohana 5:28-29).Njia tunayotakiwa kuifuta ili kuufikia uzima wa milele ni njia ya Yesu Kristo peke yake naye anasema hivi;Yohana 14:6 “Yesu akamwambia (Tomaso),Mimi ndimi njia, na kweli na uzima, mtu haji kwa Baba ,ila kwa njia ya mimi, “Yesu wakati anazungumza na Martha baada ya Lazaro kufa Yesu akamwambia ,Mimi ndimi huo ufufuo na uzima .Yeye aniaminiye mimi ajapokufa atakuwa anaishi naye kila aishiye;na kuniamini hatakufa kabisa hata milele (Yohana 11:25-26)”.
Katika sehemu hii ya tatu ya Neno hili tuangalie maana ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.Tuangalie kwa jinsi gani Mungu ametupa ujuzi wa kutambua mema na mabaya na hatimaye kufanya uchaguzi sahihi. Mungu aliwaumba Adamu na Hawa kwa mfano wake wawe huru wakiwa na uwezo wa kufanya maamuzi, uwezo wa kuchagua mema na mabaya.Mungu alikuwa wazi kwao kwa kuwaonyesha waziwazi matunda ambayo wanaruhusiwa kula na yale ambayo hawaruhusiwi.Vivyo hivyo Mungu amekuwa wazi kwetu sisi kwa kutuonyesha wazi wazi mambo mema yanayompendeza Yeye na mambo mabaya ambayo ni chukizo mbele ya uso wake.Tuanze kwa kuangalia mambo ambayo ni chukizombele ya uso wa BWANA Mungu wetu .Dhambi yoyote ilenichukizo mbele ya Mungu.Mungu ametupa amri zake kumi na kututaka kuzishika na kuzitii.Katika Neno lake takatifu tunapata mausia mengi kuhusu mambo ambayo ni chukizo kwa Mungu. .Hapa tutaona mifano michache tu kwani orodha ni ndefu mno.Wagalatia 5:19-2. “Basi matendo ya mwili ni dhahiri ndiyo haya, uasherati,uchafu ,ufisadi,ibada ya sanamu,uchawi, uadui, ugomvi,wivu,hasira,fitina,faraka,uzushi,husuda, ulevi,ulafi na mambo yanayofanana na hayo,
katika hayo nawaambia ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. “Katika Mithali 6:16-19 “Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA Naam viko saba vilivyo chukizo kwake. Macho ya kiburi,ulimi wa uongo na mikono imwagayo damu isiyo na hatia.Moyo uwazao mawazo mabaya, miguu iliyomwepesi kukimbilia maovu.Shahidi wa uongo asemaye uongo naye apandaye mbegu za fitina kati ya
Tuangalie mambo mema yanayompendza Mungu wetu.Mambo yanayompendeza Mungu ni mengi sana lakini hapa tutaangalia mambo machache tu.Kuishi kwa unyoofu wa moyo na kutenda mema ni jambo linalompendeza Mungu. 2Wafalme 20:3-6 Mfalme Hezekia alikwenda mbele za Mungu katika kweli na kwa moyo mkamilifu na kutenda yaliyomema machoni pake. “Nakusihi BWANA, ukumbuke sasa jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana”Tabitha aliyeitwa Dorcas alikuwa amejaa matendo mema na Mungu akamfufua kutoka wafu. Matendo ya Mitume 9:36 “ Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri
yake ni Dorkasi ( yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema nasadaka alizotoa “Alipokufa Petro akamwomba Mungu na Mungu akamfufua akawa hai tena. Tukiishi maisha matakatifu na kuenenda katika Bwana Yesu tutampendeza Mungu.Kwa maana tu kazi yake tuliumbwa katika Kristo,tutende matendo mema ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende
nayo Waafeso 4:1-4. “Kwa hiyo nawasihi mimi niliye mfungwa katika Bwana mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa, kwa unyenyekevu wote na upole ,kwa uvumilivu mkichukuliana katika upendo na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani, Mwili mmoja, na Roho mmoja kama mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. “Wakolosai 3:16-17,20 “ Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi na nyimbo na tenzi za rohoni huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.Na kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.Ninyi watoto watiini wazazi wenu katika mambo yote maana jambo hili lapendeza katika Bwana”.
Mambo haya yote hatuyawezi ipasavyo bila kumkubali na kumwalika Roho Mtakatifu katika maisha yetu kwa kuwa yeye atatufundisha kweli yote .Roho Mtakatifu yuko tayari kutusaidia katika kutenda mambo mema yanayompendeza Mungu.Ni jukumu letu sisi kumpa nafasi hiyo na kutambua kwamba bila msaada wake sisi hatuwezi lolote .Waafeso 2:8 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu ni kipawa cha Mungu wala si kwa matendo mtu awaye yote asije akajisifu”.
Neema na iwe pamoja nanyi nyote mnaompendeza Mungu kwa kutambua mema na mabaya na kuishi katika kutenda mambo mema kwa utukufu wa BWANA Mungu wetu.
Baada ya kujua mema na mabaya ni wajibu wetu kufanya uchaguzi sahihi wa njia ya kufuata, aidha ile ya mti wa uzima au ya jehanamu .Kumbukumbu la Torati 30:19 “ Nazishuhudia mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, Baraka na laana ; basi chagua uzima , ili uwe hai wewe na uzao wako”. Uzima na mauti Baraka na laana, vimewekwa mbele zako daima ni kazi yako kuchagua sio ya Mungu kukuchagulia.
Ufunuo wa Yohana 3:20-22 “Tazama nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia
sauti yangu , na kufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye,
na yeye pamoja nami. Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti
changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika
kiti chake cha enzi yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho
anayaambia makanisa”.