• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
  • 13 Oct, 2023
  • Admin

ZABURI 31:19 “Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako ulizowawekea wakuchao, ulizowatendea wakukimbiliao mbele ya wanadamu”.

ZABURI 31:21 “Bwana ahimidiwe, kwa maana amenitendea fadhili za ajabu katika mji wenye boma.

ZABURI 32:7   Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso, utanizungusha nyimbo za wokovu.


Mwimba Zaburi hizi anaonyesha kuwa Mungu ni mwenye fadhili nyingi ambazo ameziweka kwa ajili ya wale wamchao na huziachilia kwa wale wamkimbiliao. BWANA amejaa huruma na neema, haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili Ee nafsi yangu umhimidi BWANA, wala usizisahau fadhili zake zote. Hakika fadhili za Mungu ni za ajabu na tena hazichunguziki kwa macho ya kibinadamu .Tuangalie mifano michahce ya fadhili hizo; Zaburi 103:3-5, 10-14, “Akusamehe maovu yako yote, akuponye magonjwa yako yote, aukomboe uhai wako na kaburi, akutie taji ya fadhili na rehema.Aushibishe mema uzee wako, ujana wako ukarejezwa kama tai. Hakututenda sawa sawa na hatia zetu, wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, kadri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. Kwa maana yeye anatujua umbo letu, na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi. “Akatuokoa na watesi wetu; na kila chenye mwili akipa chakula chake kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuru BWANA kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuru BWANA kwa maana fadhili zake ni za milele.

Kwa kuwa fadhili zake ametuwekea hatuna budi kumkimbilia ili atupe fadhili hizo.Zaburi 46:1-11 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. “ Enyi watu, mtumainini siku zote ifunueni mioyo yenu mbele zake, Mungu ndiye kimbilio letu .Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza, hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele. Lakini wewe BWANA, U BWANA wa rehema na neema. Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli, unielekee na kunifadhili mimi.  

Tukishamkimbilia Mungu tuhakikishe kuwa tunajificha katika mbawa zake. Zaburi 32:7-10 “Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso, utanizungusha nyimbo za wokovu (You are my hiding place, you will preserve me from trouble you will surround me with songs of deliverance). Mungu akituficha katika mbawa zake shetani hataweza kutusogelea wala kutuangamiza .Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka .BWANA atakuwa ngome kwake aliyeonewa, Naam, ngome kwa nyakati za shida Zaburi 27:5 “ Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, atanisitirikatika sitara ya hema yake na kuniinua juu ya mwamba” Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu; unikomboe, unifadhili . Mithali 18:10 “Jina la BWANA ni ngome imara, mwenye haki huikimbilia akawa salama”. Mungu anasema kuwa tutamuona tutakapo kiri kwa midomo yetu na kusema kwamba, “Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana,” na hapo ndipo atakapokusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku akusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake. BWANA atakapotuosha uchafu wote na kuwa watakatifu ndipo BWANA ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku, kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua (Isaya 4; 5). Siku zote uwe na uhakika kuwa Yesu ndiye mwamba wa kale, kuhani wa milele, ndiye mfalme wa amani, ndiye jiwe kuu la pembeni ndiye msingi, ndiye wa kanisa. Ufunuo 17:14 “ Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme na hao walio pamoja naye ndio walioitwa , na wateule, na waaminifu”.

Share This