• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
  • 10 Mar, 2024
  • Admin

KUMSHUKURU MUNGU KWA MOYO WAKO WOTE

Kumshukuru Mungu kwa moyo wako wote maana yake ni nini? Kuna njia mbili za kushukuru  unaweza kushukuru kwa maneno  na vitendo vya nje ambavyo humaanishi ni kama kiili macho au kama kawaida  ya mtu  akitendewa jambo jema.  Shukrani za aina ya pili ni zile zinazotoka ndani ya myo wako .Maneno na vitendo vyako vya shukrani vinasukumwa  na moyo wako au tusema ni shukrani inayoanzia  moyoni ndio viashiria  vya nje vitokee kama vile kicheko, furaha  na mashangilio. Hizi ndizo shukrani zinazompendeza Mungu. Mungu humpenda  yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu (2 Wakorintho 9:7). Tutoe shukran kwa Mungu kwa moyo wa kupenda wala sio wa kulazimishwa au kushurutishwa au kwa masharti yoyote yale. 2 Wakorintho 9:7 “Kila mtu na atende kama alivyokusudia  moyoni mwake  si kwa huzuni wala si kwa lazima,Maana Mungu humpenda yeye atoaye shukrani  kwa moyo wa ukunjufu”. Mtu anayetoa kwa moyo wa ukunjufu  anampenda Mungu kwa moyo wake  wote .Neno la Mungu katika Luka 10:27(a) linasema “akajibu akawambia,(Yesu Kristo),Mpende Bwana Mungu wako  kwa moyo wako wote.”Moyo wa shukrani ni moyo unaomrudishia Mungu utukufu na heshima zote.Ukiwa na moyo wa shukrani utajikuta unamwinua Mungu kwa kuelezea kwa watu  na makutano juu ya uweza wake  na nguvu  zake  na matendo yake makuu na ya ajabu. Zab:35-18. “Nitashukuru katika kusanyiko kubwa, nitakusifu kati ya watu wengi.” Na sisi kama Daudi tumshukuru Mungu kati ya watu na kati ya mataifa. Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu  maana yeye atatuwesha .Jina la BWANA Lihimidiwe tangu leo na hata milele.

 

Share This