• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
  • 30 Aug, 2023
  • Shaidi Nziamwe

Shaidi alizaliwa katika karne ya 19 na kuwa mmoja wa watoto watano wa Nziamwe na mkewe Nakusighe, aliyebatizwa na kuitwa Uzeeli. Shaidi alikuwa na ndugu zake, Madafa, Lukwaro, Ishundi, na Yofika. Shaidi alimuoa Kompeho Msangi Narundu (Nashamwa) kutoka Chome. Kompeho alikuwa mkulima hodari aliyelea na kusimamia familia yake vizuri. Kompeho alifahamika sana kwa ukarimu wake hasa kwa familia zenye shida. Wakati wa njaa alisaidia familia nyingi zenye shida ya chakula kwa kuwapa chakula. Inasemekana kuwa hakuna familia iliyolala njaa wakati wake kwa kuwa alikuwa tayari kutoa kidogo alichonacho kwa ajili ya wengine. Kompelo pia alikuwa mkunga wa jadi maarufu katika eneo la Vudee ambaye aliwasaidia wakina mama wengi wakati wa kujifungua.

FAMILIA YA SHAIDI NZIAMWE 

Mungu alimjalia Shaidi na mkewe Kompeho watoto saba (7) wa kiume  na watoto (4) wa kike kama ifuatavyo:- 

1. Ghuheni (Nziamwe) 

2. Elangwa Msangi Narundu 

3. Abraham (Madafa) 

4. Mkunde (Nakusighe)

5. Paulo(Lukwaro) 

6. Marko Chalambo  (Kaghembe)  

7. Naza - alifariki akiwa  msichana wa miaka 14 

8. Enikunda (Namhezi) 

9.Naomba- alifariki akiwa  msichana wa miaka 16 

10.Yonazi 

11.Elifadhili(Ishundi) 

*Majina kwenye mabano ni majina ya babu au bibi zao. Katika familia za  Kipare mtoto akizaliwa hupewa jina la babu au bibi yake.

Hii ni picha ya mchoro wa nyumba ya Shaidi Nziamwe. Ilikuwa miongoni mwa nyumba za kwanza kijijini vudee kuwa na vyumba vya juu.

17009970440.png

Pia Shaidi Nziamwe alishiriki kwenye ujenzi wa nyumba wachungaji vudee inayo onekana kwenye picha hapa chini

 17009970441.png 17009970442.png