• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
  • 23 Aug, 2023
  • Admin

Updates za Mkutano wa Injili 2022

  • Bwana Yesu asifiwe.Mkutano wa Injili umefungulia leo na Mhe.Baba Askofu Charles Mjema.Mhe.Baba Askofu ameweka wakfu vyombo tulivyonunua kwa ajili ya mikutano ya Injili.Tunamshukuru Mungu kwa kutupatia vyombo vitakavyotumika kwa utukufu wake.
  • Bwana Yesu asifiwe sana wapendwa. Tunamshukuru sana Mungu wetu tunaendelea na mkutano wetu wa injili katika vituo vya Vudee kati na Kwainka.Muitikio ni mzuri,lkn pia asubuhi tunaendelea kushuhudia nyumba kwa nyumba.Niwaombe tuendelee kuumbea mkutano huu ili uweze kumzalia Mungu matunda.
  • Shalom shalom wapendwa, tunamshukuru sana Mungu jana tumefungua mkutano katika kituo cha Ndolwa na mkutano ulikuwa mzuri sana.Tuendelee kuuombea mkutano wetu.Wapendwa Bwana Yesu asifiwe.Tunamshukuru Mungu leo ni siku ya tano ya mkutano wetu Ndolwa.Mungu anaendelea kuhudumia watu wake nasi tunalihimidi Jina lake takatifu.Ninawashukuru wote waliotoa fedha zao na wanaoendelea kutoa kufanikisha mkutano huu wa Injili.Tuendelee kumwomba Mungu aonekane kwa viwango vikubwa.Furahieni pamoja nasi sifa hizi kwa BWANA.
  • Nawasalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.Watu wa Ndolwa pamoja na sisi sote tunatakiwa tuchague hivi leo tutamtumikia nani.Yoshua yeye anasema lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA
    Tunamshukuru sana Mungu wetu kwa kuwa leo tumemaliza mkutano wetu Ndolwa kwa amani na furaha na mashangilio.Tumemwona BWANA akitenda kazi katikati yetu.Jina la BWANA lihimidiwe.

TAARIFA  YA MKUTANO WA INJILI VUDEE- SEPT 2022

Shalom ndugu wapedwa Wacharo. Nawasalimu kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Naomba kuwasilisha taarifa ya kikao cha kwanza cha Wacharo baada ya mkutano wa injili Vudee kwa mwaka 2022. Kikao chetu kilifanyika kama kilivyopangwa na Mungu awabariki wajumbe wote waliohudhuria.

1. Katika kikao hicho taarifa ya fedha za mkutano wa Injili Vudee wa Sept. 2022 ilitolewa na kujadiliwa. Fedha iliyobaki iliamuliwa itumike kulipia stabilizer ya KVA 10 ambayo ni kubwa zaidi itakayostahimili vifaa tulivyo navyo. Tuliyokuwa nayo ya 5 kva iliungua wakati wa mkutano. Tunamshukuru sana Mungu aliyewezesha mkutano wa injili Vudee kwa mwaka huu kufanyika kwa mfanikio makubwa. Taarifa ya mapato na matumizi imeambatishwa. Tunawashukuru wote waliochangia mkutano wa Injili Vudee. Mungu wa Mbinguni awabariki sana.

2. Taarifa yà vyombo vya muziki na michango ya zahanati ya KKKT Vudee itatolewa baadae mwezi huu. Tunamwomba Mungu wacharo wote tupate neema ya kuchota baraka ya kushiriki katika shughuli za Kanisa nyumbani Usharikani kwetu.

MUNGU AWABARIKI MNAPOENDELEA NA KIPINDI CHA MAAJILIO.

Picha, Budget pamoja na viambatanisho vingine vya tukio hili vinapatikana kwa kubovya link hii- BOFYA HAPA



Share This