TAARIFA YA MKUTANO WA INJILI USHARIKA WA VUDEE – 2021
Bwana Yesu Asifiwe.
Ifuatayo ni taarifa ya mkutano wetu wa Injili katika ushirika wa Vudee uliofanyika tarehe 12/09/2021 hadi 19/09/2021. Mkutano wetu wa mwaka 2021 ulifanyika katika vituo vitatu.
1. Vudee Kati
2. Ndolwa
3. Kwainka
- Mkutano wa mwaka 2021 tuliongozwa na neno kutoka INJILI YA YOHANA 17:3 “NA UZIMA WA MILELE NDIO HUU WAKUJUE WEWE, MUNGU PEKEE WA KWELI, NA YESU KRISTO ULIYEMTUMA”
- Ndugu mwenyekiti na wajumbe/vacharo. Mkutano wetu ulikuwa na wanenaji watatu na waimbaji binafsi wawili.
Wanenaji ni mwinjilisti
1. Jonas Bwemelo
2. Damian Ndelwa
3. Kiariro Mkilindi
Waimbaji
1. Christina Mbilinyi
2. Tina Mnzava
- Mkutano wetu uliweza kufanyika kwa utulivu na amani, mwitikio na mahudhurio yalikuwa ya kutosha na watu wengi waliokoka na kuombewa uponyaji na kufunguliwa.
- Katika vituo vyote vitatu tuliweza kumtolea Mungu sadaka zetu za shukrani.
- Vacharo katika Fellowship zao walitoa sadaka zao na zilielekezwa kuwatunza watumishi wa usharika. Pia tulipokea sadaka ya vitambaa kwa ajili ya huduma
- Mkutano wetu wa injili mwaka huu ulifunguliwa na kufungwa na msaidizi wa Askofu, Mchungaji Ibrahim Azayo Ndekia.
- Ndugu mwenyekiti na wajumbe/vacharo mkutano wetu ulikumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo usafiri wa pikipiki na vyombo vya mziki.
- Ndugu mwenyekiti na wajumbe/vacharo taarifa hii imeambatanishwa na taarifa ya fedha na matumizi, karibuni kwa ajili ya kuijadili na kufanya tathimini ya mkutano wetu wa mwaka 2021 kwa lengo la kuona jinsi ya kuboresha mwaka 2022.