MKUTANO WA INJILI VUDEE NA NDOLWA 2020-(13/9-20/9/2020)
UTANGULIZI
Wanawake kulingana na neno la Mungu wana nguvu kubwa sana wamepewa uwezo wa kipekee ambao wakiugundua na kuutumia vyema watafika mbali katika ndoto na malengo yao.Kila mwanamke wa Vudee akiitambua nguvu hii na kusimama kwenye nafasi yake kwa uhodari bila woga wowote ataweza kulijenga kanisa la Mungu .Semina hizi zinalenga katika kuwafundisha wanawake uwezo wa Mungu uliopo ndani yao na jinsi ya kuutumia kujenga kanisa la Mungu.Vijana wa Vudee wana shida moja kubwa ya kutohudhuria makanisani .Vijana wengi wakishapata kipaimara huwaonekani tena makanisani. Kuna haja kubwa ya kuimarisha imani yao kwa Mungu kwa njia hii ya semina.Semina hizi zinalenga katika kuwafundisha vijana kuhusu ufalme wa mbinguni na jinsi unayopatikana.Wana semina wanatakiwa wawe chachu na mbegu kwa vijana wengine.
1. Semina ya wanawake (Vudee na Ndolwa)
Somo: Mwanamke shupavu na shujaa simama katika nafasi yako umtumikie Mungu na ulijenga kanisa lake.
Neno:Zaburi 68:11 Bwana analitoa neno lake, wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa.
1.1 MAFUNDISHO;
· Katika somo hili watajifunza kutoka kwa wanawake shupavu na mashujaa katika Israeli (Maria,Debora,Ruth,Esta,Abigaili, Hana,Yaeli,nk).
· Watajifunza kuhusu mbinu na nguvu za kijeshi ziletazo ushindi (Upendo,utii,unyeyekevu na jina la Yesu ) Mithali 14:1,Wimbo ulio Bora 8:6-7,1Samweli 15:22-23,Wakolosai 3:18-19,1Petro 5:5
· Watajifunza kuhusu habari zinazotakiwa kutangazwa katika kanisa la Mungu (Isaya 61:1,20:17-18, Zaburi 96:2 Luka 4:18-19,1Petro 2:9-10
· Watajifunza kuhusu wanawake shupavu na mashujaa katika nchi ya Vudee (wasaidizi, wazazi,walezi, walinzi ,wahubiri na waombaji. Yote hayo yanahitaji ushupavu mkubwa.Dondoo hii inaweza kujadiliwa katika vikundi.
2. Semina ya Vijana (Vudee na Ndolwa)
Somo: Ufalme wa mbinguni hutekwa na wenye nguvu.
Neno: Mathayo 11:12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu ,nao wenye nguvu wauteka.
Kichwa kidogo cha somo;
1Yohana 2:14 (b) Nimewaandikia ninyi vijana kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
2.1 MAFUNDISHO
· Watajifunza kuhusu maana ya ufalme wa mbinguni (Mathayo 22:1-14 ,Marko 9:1,Yohana 3:5).
· Watajifunza mbinu za kuuteka ufalme wa mbinguni (1Yohana 1:9,Waefeso 6:17,
2 Timotheo 1:7)
· Watajifunza kuhusu nguvu inayohitajika kuuteka ufalme wa mbinguni na kumshinda yule mwovu (Isaya 40:29-31,Wakolosai 3:16 ,Yohana 1:12, 1Waebrania 4:12)
· Watajifunza kuhusu nguvu iliyoko ndani ya vijana na jinsi ambavyo neno la Mungu linakaa ndani yao (Wagalatia 33:26,Wakolosai 3:16)
· Wataangalia jinsi vijana wa Vudee/Ndolwa wanavyotumia nguvu zao katika kuuteka ufalme wa mbinguni. (Wakolosai 4:5-6, Mhubiri 12:1,Waefeso 5:15-21,
1 Wathesalonika 4:11-12, Waefeso 4:29) Dondoo hii inaweza kujadiliwa katika vikundi
3.0 WAALIMU
Watakaofundisha masomo haya ni wanenaji wa mkutano wa Injili Vudee-2020 .Wanenaji watajipanga jinsi watakavyohudumu katika vituo hivyo viwili kulingana na ratiba ya mkutano .Dondoo hizi pamoja na zingine zitasaidia katika kukamilisha semina hizi kwa utukufu wa Mungu.Tumpe nafasi na tumwombe Roho Mtakatifu atufundishe sawasawa na mapenzi ya Mungu.